STEM

Miaka 50 baada ya walioenda mwezini kutua ardhini, UN bado inaunga mkono harakati

“Sisi wakazi wa dunia, ambao tunaweza kutatua matatizo ya sayari hii, tunaweza kutatua matatizo  yatokanayo na kuishi kwenye sayari hii,” ni kauli yake Neil Armstrong, binadamu wa kwanza kufika mwezini, kauli ambayo alitoa mara baada ya kutembelea Umoja wa Mataifa wiki tatu baada ya safari yao hiyo ya kipekee.

Binti mwenye umri wa miaka 16 nchini Tanzania atengeneza Apu ya kusaidia wanawake wajawazito kufuatilia hali zao.

Sauti za wanawake na wasichana na ujuzi katika sayansi, teknolojia na ubunifu ni muhimu katika kuleta suluhu katika dunia ya sasa ambayo inashuhudia mabadiliko ikiwemo mabadiliko haribifu, yanasisitiza mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la wanawawake yaani UN Women na lile la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.

 

Nguvu ya vijana wa bara la Afrika, zinaendeleza bara hilo kuelekea enzi mpya za maendeleo endelevu-Antonio Guterres.

Nguvu na matumaini ya vijana isiyo na mipaka ya vijana wa kiafirika vinaimarisha bara hilo kuelekea katika nyakati mpya za maendeleo endelevu, sambamba na ushirikiano mpya kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, AU. Hiyo ni kwa mujibu wa ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alioutoa hii leo katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Afrika.

Zaidi ya kuwa mhandisi, Nadhifa Zubeir ni mama na mke

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, katika masomo ya ngazi ya juu takribani asilimia 30 pekee ya wanafunzi wa kike ndiyo wanachagua masomo yanayohusiana na sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.

Sauti -
3'19"

Mchango wa wanawake na wasichana katika sayansi ni muhimu sana:UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amehimiza haja ya kuziba pengo la wanawake na wasichana lililopo katika nyanja ya sayansi, uhandizi na hisabati au STEM akisema mchango wao ni mkubwa na unahitajika.

Sauti -
1'21"

11 Februari 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Siku ya kimataifa ya wanawake na wasicha katika sayansi , mchango wa kundi hili ni muhimu asema Katibu Mkuu Antonio Guterres

Sauti -
11'14"

Wanasayansi wasichana wa Afrika wako mstari wa mbele katika vita ya kuleta usawa wa kijinsia katika sayansi-Antonio Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo hii mjini Addis Ababa Ethiopia amekutana na kuzungumza na wasichana kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambao wanashiriki katika mpango wa kuwafanya kubobea katika programu za kompyuta, mkakati wa unaoratibiwa kwa pamoja kati ya Muungano wa kimataifa wa Mawasilino (ITU) na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women.

Udadisi wangu ulisababisha wanishawishi nijikite kwenye masomo ya sayansi-Mhandisi Nadhifa

Katika makala kwa kina ya wiki hii  Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam anazungumza na mhandisi wa ndege katika shirika la ndege la Tanzania ATCL,  Nadhifa Zubeir Hassan kuhusu kazi hiyo ya ufundi wa ndege.

Sauti -
5'