Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 MEI 2023

08 MEI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tanaangazia Jukwaa la Umoja wa Mataifa la misitu linaloendelea hapa makao makuu, vita dhidi ya ukimwi Moldova. Makala tunakupeleka nchini Uganda na Mashinani nchini Rwanda, kulikoni?

  1. Jukwaa la 18 la Umoja wa Mataifa la misitu limeanza leo kwenye makao Makuu ya Umoja huo mjini New York Marekani likiwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mfumo wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa na kikanda na wadau wa misitu ili kujadili thamani ya rasilimali hiyo muhimu kwa binadamu na mazingira.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na vita dhidi ya ukimwi UNAIDS limesema ili kuhakikisha ukimwi unatokomezwa ifikapo mwaka 2030 basi kila mtu anapaswa kujumuishwa katika vita hiyo ikiwemo wafungwa na wanaotumia mihadarati, kwani mifumo mingi ya magereza inajitahidi kukabiliana na msongamano, rasilimali duni, ufikiaji mdogo wa huduma za afya na huduma zingine za msingi, vurugu na matumizi ya dawa za kulevya.
  3. Makala inatupeleka Uganda kumulika juhudi zinazofanywa na shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kupambana na malaria.
  4. Mashinani tutaeleke nchini Rwanda kumsikia mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa ana matumaini baada ya kupokea msaada wa kibinadamu.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
13'32"