Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 MACHI 2023

13 MACHI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia hitimisho la ziara ya Baraza la Usalama DRC na UN Global Compact Tanzania. Makala tutasalia tunakurejesha hap makao makuu katika mkutano wa CSW67 na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

  1. Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametamatisha ziara yao ya siku tatu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC iliyolenga kujadili kwa kina majukumu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO halikadhalika kujionea hali halisi ya amani na usalama.
  2. Nchini Tanzania Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kushirikisha kampuni kuzingatia será na misingi endelevu na inayojali jamii, au kwa kiingereza UN Global Compact Tanzania umeanza kuona mabadiliko katika kushirikisha kampuni kuzingatia misingi 7 ya kumwezesha mwanamke kwenye sekta ya biashara.
  3. Makala inaturejesha hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani SCW iumeingia wiki ya pili na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amepata fursa ya kuzungumza na mbunge anayewakilisha asasi za kiraia kutoka Tanzania Neema Lugangira ambaye anashiriki mkutano huo wa kikao cha 67 kuhusu mada kuu ya kikao hicho ubunifu na teknolojia katika kusongesha mbele maendeleo ya wanawake akitaka kufahamu suala hilo linapewa uzito gani Tanzania.
  4. Na mashinani tutasikia ujumbe kuhusu unyanyasaji wa kijinsia utokanao na  mfumo dume ambao bado  umesalia kuwa kikwazo cha maendeleo katika nchi nyingi duniani.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'6"