Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 Desemba 2022

27 Desemba 2022

Pakua

Hii leo katika jarida la Umoja wa Mataifa utasikia mada kwa kina kuhusu utalii endelevu nakulinda wanyamapori walio hatarini kutoweka nchini Tanzania.

pia utasikia habari kwa ufupi kuhusu marufuku ya wanawake nchini Afghanistan kufanya kazi kwenye NGOs, Wakimbizi waliokwama baharini kwa mwezi mzima waokolewa na Indonesia na Wakimbizi wa ndani nchini Ukraine wapatiwa msaada katika msimu huu wa baridi. 

Na tukiwa bado kwenye msimu wa sikukuu, wakimbizi kutoka nchini Ukriane wanajaribu kufanya kila jitihada kuhakikisha nao wanasherehekea sikukuu hizi.

Sekta ya utalii ni miongoni mwa sekta zenye mchango mkubwa katika malengo ya maendeleo endelevu SDG’s huku Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo sekta hiyo kuwa endelevu kwa maslahi ya dunia na watu wake. Nchini Tanzania vijana wanaichangamkia sekta hiyo kwanza kama chanzo cha ajira lakini pia kuchangia katika uchumi wa taifa na jamii zinazowazungukaa. Miongoni mwa vijana hao ni Steven Ngowi anayemiliki kampuni ya utalii ya NDIFO Safari, ambaye mbali ya kuwa muongoza watalii anachagia katika miradi mbalimbali ya jamii na kusaidia kuokoa wanyama walio hatarini kutoweka . Hivi karibuni alifika hapa Marekani kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanyama hao walio hatarini kutoweka wakiwemo tembo. Amezungumza na Flora Nducha wa na kufafanua ni kwa jinsi gani wanavyosaidia wanyama hao walio hatarini kutoweka.

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
13'5"