Ripoti ya UNODC: Licha ya juhudi kubwa, ujangili wa wanyamapori bado unaendelea
Licha ya juhudi zinazoendelea kufanyika ulimwenguni kwa takriban miongo miwili zaidi ya aina 4,000 za wanyamapori wenye thamani bado wanakabiliwa na ujangili kila mwaka, hii ni kulingana na ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la dawa na uhalifu, UNODC.