30 DESEMBA 2020
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea matukio ya mwaka 2020
-Mwaka 2020 ulitangazwa kuwa mwaka wa wauguzi na wakunga na shirika la afya duniani WHO
-Janga la corona au COVID-19 Machi mwaka huu lilitangazwa kuwa janga la kimataifa. Na kwa mujibu wa WHO nchi 222 duniani zimeathirika huku watu zaidi ya milioni 1 na laki 7 wakipoteza maisha na wengine zaidi ya milioni 79 wameambukizwa ugonjwa huo