Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni lazima vijana washirikishwe majadiliano ya SDGs-Rita

Ni lazima vijana washirikishwe majadiliano ya SDGs-Rita

Pakua

Vijana wana mchango mkubwa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endevu yaani SDGs kwa sababu ya msukumo na ubunifu wao’ hiyo ni kauli ya Rita Kimani, kijana kutoka Kenya ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya FarmDrive nchini humo  inayosaidia kuunganisha wakulima wadogo wadogo na fursa za mikopo bila kuhitaji dhamana.

Pia yeye ni mmoja wa viongozi vijana wa Umoja wa Mataifa wanaosongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Akihudhuria  mkutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa alipata fursa ya kuzungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii kuhusu afanyacho na umuhimu wa vijana katika ajenda ya maendeleo. Ungana nao katika sehemu hii ya kwanza ya mahojiano, Rita anaanza kwa kulezea umuhimu wa vijana kushiriki meza ya mazungumzo kuhusu masuala ya SDGs.

Photo Credit
Kijana Rita Kimani wa FarmDrive kutoka Kenya alipohojiwa na UN News Kiswahili. Picha na UN News Kiswahili/Patrick Newman.