Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado kuna watoto milioni 152 wanatumikishwa katika ajira duniani:ILO

Bado kuna watoto milioni 152 wanatumikishwa katika ajira duniani:ILO

Pakua

[caption id="attachment_332032" align="aligncenter" width="625"]03hapanapaleiloajirawatoto

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO Guy Ryder ameonya kwamba bado kuna watoto milioni 152 ambao ni wahanga wa ajira ya watoto kote duniani .

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa kimataifa wa kutokomeza ajira ya watoto duniani mjini Buenos Aires, Argentina , ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana ili kufikia lengo la kutokomeza kabisa ajira ya watoto ifikapo mwaka 2025.

Amesema hata hivyo kuna hatua zimepigwa katika miaka 20 iliyopita katika kupunguza tatizo hilo japo ameonya kwamba bado safari ni ndefu ya kuondokana kabisa na mifumo yote ya utumikishwaji wa watoto.

Kwa mujibu wa ILO karibu nusu ya watoto hao milioni 152 sawa na mtoto mmoja kati ya 10 wako katika ajira za hatari huku milioni 25 wakiwa katika ajira za shuruti.

Mkutano huo utakaomaliza kesho umeandaliwa na wizara ya kazi, ajira na usawi wa jamii ya Agentina kwa msaada wa ILO.

Photo Credit