Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Keating ajadilia amani na usalama na wanawake viongozi Somalia

Keating ajadilia amani na usalama na wanawake viongozi Somalia

Pakua

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa mpango wa Umoja huo nchini Somalia UNSOM Michael Keating, leo amekuwa mwenyeji wa mkutano wa wanawake viongozi wa Somalia kuzungumzia azimio nambari 1325 la baraza la usalama kuhusu wanawake, amani na usalama.

Amessisitiza kwamba mchango wao na wanawake wengine katika jamii ni muhimu hasa katika kuleta amani, kuzuia na kutatua migogoro, kujadili amani, na kuzuia na kulinda wanawake na wasichana dhidi ya vita.

Amewaambia ni muhimu sana wao kushiriki sawia katika masuala mbalimbali ikiwemo juhudi zenye lengo la kuleta amani ya kudumu na usalama nchini humo baada ya zaidi ya miongo miwili ya vita.

Amesema cha msingi kwa wanawake hao ni kujiuliza ni kwa jinsi gani wanawaweza kugeuza dhana hiyo iweze kuzaa matunda huku akiwakumbusha kwamba wana wajibu kwa waliopoteza maisha, waliojeruhiwa na wanaoendelea kukabiliwa na madhila, ili kuhakikisha wanaondokana na madhila hayo kwa kufikia amani na usalama wa kudumu akiwahakikishia ana imani nao asilimia 100 kwamba wanaweza kutekeleza hilo.

Photo Credit
Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNSOM Michael Keating, ni mwenyeji wa mkutano wa wanawake viongozi wa Somalia. Picha: UNSOM