Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres akutana na Aung San Suu Kyi huko Manila

Guterres akutana na Aung San Suu Kyi huko Manila

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko ziarani barani Asia amekuwa na mazungumzo na kiongozi mkuu wa Myanmar, Daw Aung San Suu Kyi.

Mazungumzo hayo yamefanyika huko Manila, Ufilipino, kando mwa kikao cha viongozi wa umoja wa nchi za kusini na mashariki mwa Asia, ASEAN.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema viongozi hao wawili wamejadili hali katika jimbo la Rakhine wakati huu ambapo mamia ya maelfu ya warohingya wa madhehebu ya kiislamu wanakimbilia Bangladesh kutokana na mateso.

Katibu Mkuu ameangazia umuhimu wa kuimarisha jitihada kuhakikisha huduma za kibinadamu zinawafikia warohingya na vile vile wakirejea nyumbani waweze kuishi maisha yenye utu bila kusahau maridhiano baina ya jamii.

Bwana Guterres pia amesisitiza umuhimu wa kutekeleza mapendekezo ya tume ya ushauri ya Rakhine iliyokuwa inaongozwa na Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.

Photo Credit
WaRohingya wana wasiwasi kufuatia mashambulizi yaliyofanyinka katika eneo la nchini Myanmar. Picha: UM