Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maiti 26 za wanawake waliosafirishwa kiharamu zawasili Italia:IOM

Maiti 26 za wanawake waliosafirishwa kiharamu zawasili Italia:IOM

Pakua

Maiti za wanawake 26 wanaosadikiwa kufanya safari ya kuelekea barani Ulaya kwa kupitia wasafirishaji haramu zimewasili nchini Italia, huku idadi ya wahamiaji kwa mwaka huu 2017 ikikarinia 155,000 na vifo Zaidi ya 2900.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, likisema asilimia 70 ya wahamiaji hao wamewasili Italia na waliosalia wameingia Ugiriki na Hispania.

IOM inasema idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na wahamiaji na wakimbizi 337,773 waliowasili Ulaya mwaka jana kufikia kipindi kama hiki.

Photo Credit
Meli za usafirishaji wa wahamiaji na waokoaji Mediterranan. Picha: IOM