Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufanikisha SDG’s lazima tuwekeze katika viwanda na ujasiriliamali:UNIDO

Kufanikisha SDG’s lazima tuwekeze katika viwanda na ujasiriliamali:UNIDO

Pakua

Uwekezaji katika ujasiriamali ni muhimu katika kufanikisha lengo nambari 9 la maendeleo endelevu la kuwa na miundombinu imara, kuchagiza viwanda endelevu na kukuza ubunifu, amesema leo naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO, Hiroshi Kuniyoshi.

Akizungumza na UN News katika jukwaa la kimataifa la uwekezaji katika ujasirialia mali kwa ajili ya maendeleo mwaka 2017 nchini Bahrain amesema lengo kuu la jukwaa hilo ni kuzihamasisha nchi katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDG’s kupitia ujasiriliamali na ubunifu, na kutathimini jinsi gani malengo hayo yatatimizwa hususani lengo nambari 9, kwa kushirikisha wadau wote zikiwemo sekta binafsi, wajasiriliamali, sekta za umma na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Amesema hivi sasa UNIDO imeshaanza mikakati

(HIROSHI CUT 1)

“Ikiwemo kuchagiza uwekezaji, kuhamisha teknolojia kutoka nchi zilizoendelea kupeleka nchi zinazoendelea, kupigia upatu mafunzo ya vitendo, kuzijengea uwezo nchi zinazoendelea na kadhalika.

Kwa upande wa vijana amewapa changamoto

(HIROSHI CUT 2)

“Kitu cha kwanza ni kufikiria kibunifu, kwa vijana bila shaka wanaweza kukabiliwa na changamoto nyingi lakini pia watakuwa na fursa , chukueni fursa hizo kujifunza jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo, na tutawapa fursa ya kujifunza.”

 

Photo Credit
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO, Bwana Hiroshi Nikiyoshi, akiwa kwenye jukwaa la uwekezaji katika ujasiriliamali kwa ajili ya maendeleo nchini Bahrain. Picha na May Yaacoub: UN News