Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kuimarisha huduma za afya ya akili nchini Somalia

Harakati za kuimarisha huduma za afya ya akili nchini Somalia

Pakua

Afya bora na Ustawi ni lengo namba 3 katika malengo ya mendeleo endevu SDGs, na Umoja wa mataifa unaendelea kusihi mataifa kote ulimwenguni kufanikisha lengo hili na kuhakikisha afya njema kwa wote ifikapo mwaka 2030.

Kwa mantiki hiyo, Umoja wa Mataifa ukishirikiana na serikali la Somalia umefanya warsha ya siku tatu mwezi Julai mwaka huu, ya kuwajenga uwezo maafisa wa afya kutoka katika taasisi za Baidoa, mji mkuu wa jimbo la Kusini mwa Somalia. Warsha hiyo ililenga kutoa maandalizi ya msingi kwa ajili ya kushughulikia ugonjwa wa akili.

Huduma za afya ya akili nchini Somalia hazijapatiwa kipaumbele kwa miaka mingi, ingawa takwimu zinaonyesha kuwa matukio ya magonjwa ya akili nchini humo ni ya juu zaidi duniani. Katika makala ifutayo, Selina Jerobon anaangazia kilichojiri katika warsha hii, ambayo ni moja ya hatua ambazo zimeachukuliwa nchini humo katika harakati za kuimarisha huduma za afya kwa jumla. Ungana naye…..

Photo Credit
Warsha ya siku tatu ya kuwajenga uwezo maafisa wa afya kutoka katika taasisi za Baidoa nchini Somalia. Picha: UM/Video capture