Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi waazimia kuboresha miundo mbinu ili kukabiliana na majanga

Viongozi waazimia kuboresha miundo mbinu ili kukabiliana na majanga

Pakua

[caption id="attachment_319082" align="aligncenter" width="625"]hapanapalemajanga2

Mkutano wa kimataifa wa kukabiliana na majanga ukiendelea mjini Cancun nchini Mexico ,viongozi wa dunia wameweka ahadi ya kufanya mapitio ya miundombinu ifikapo mwaka 2019 ili kupunguza athari za kiuchumi zitokanazo na majanga.

Viongozi hao katika hotuba zao wamesema majanga hayana mipaka, na kutaka mkakati wa Sendai kuhusu kukabiliana na majanga, umeleta mafaniko katika kupunguza majanga.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed amewaeleza washiriki wa mkutano huo wa siku sita kwamba majanga yamepungua katika nchi nyingi kutokana na kile alichokiita taasisi thaibiti na mikakati ya kisera.

Amesema uwepo wa mifumo ya tahadhari za mapema, uelewa wa majanga, kuongezeka kwa ushirikiano dhidi ya asasi za kiraia na uwajibikaji zaidi kwa majanga ya kibinadamu yamewezesha kupungua kwa majanga.

Photo Credit