Wanasayansi kutafiti maji Sahel kwa kutumia teknolojia ya nyuklia-IAEA

Wanasayansi kutafiti maji Sahel kwa kutumia teknolojia ya nyuklia-IAEA

Pakua

Katika ukanda wa jangwa la Sahel , moja ya maeneo masikini kabisa duniani maji yaliyojikita ardhini yatoa nuru ya maisha.

Wanasayansi kutoka nchi 13 za Afrika wamefanya tathimini ya kwanza kabisa ya maji yaliyo chini ya ardhi katika ukanda huo ikihusisha eneo la kilometa milioni 5 kwa msaada wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA ikitumia teknolojia ya nyuklia.

Hadi sasa wamebaini mambo kadhaa ikiwemo kiwango cha uchafuzi, mwelekeo na mtiririko wa maji unaounganisha vyanzo mbalimbali na mabonde.

Wanasayansi hao wanasema taarifa hizo ni kama dhahabu kwani sasa wanaweza kuzifahamisha serikali wapi palipo na rasilimali ya maji mbadala ili waweze kuchimba visima au maji hayo yatadumu kwa muda gani.

Beatrice Ketchemen Tandia mtaalamu wa maji na miamba wa chuo kikuu cha Douala Jamhuri ya Afrika ya Kati ambaye amekuwa akishiriki utafiti wa masuala ya maji wa IAEA tangu miaka ya 1990 amesema watu wanahitaji maji ili kuishi, na kuweza kudhibiti maji hayo unahitaji kuyaelewa.

Ukanda wa Sahel una watu takribani milioni 135 na moja ya changamoto kubwa inayowakabili ni fursa ya kupata maji safi ambayo ni muhimu kwa kunywa, kupikia, usafi na uzalishaji.

Photo Credit
Mwanasayansi akichukua sampuli ya maji huko Bangui, CAR.(Picha:L. Gil/IAEA)