Simulizi ya mama mkimbizi wa Sudan Kusini aliyeko Uganda
Pakua
Ni simulizi yenye simanzi! Familia imetawanyika kila mtu akikimbilia asikokufahamu kunusuru uhai wake. Hiyo si sehemu tu ya madhila yanayozikumba familia nyingi nchini Sudan Kusini wakati huu ambapo machafuko zaidi yanaripotiwa.
Ungana na Amina Hassan katika makala itakayokukutanisha na mama mkimbizi wa Sudan Kusini aliyekimbilia Uganda kusaka hifadhi.