Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viwavijeshi waleta hofu kusini mwa Afrika

Viwavijeshi waleta hofu kusini mwa Afrika

Pakua

Uvamizi wa viwavijeshi kwenye mashamba kusini mwa Afrika kumezua sintofahamu siyo tu kwa wakulima bali pia wataalamu wa kilimo. Hivi sasa wadudu hao waharibifu wanakula mimema na mazao hali ambayo inaleta hofu kubwa juu ya mustakhbali wa chakula katika ukanda huo ambao bado una machungu ya athari za El Nino. Je nini kinatokea na Umoja wa Mataifa unapendekeza nini? Ungana basi na Flora Nducha kwenye makala hii inayoangazia shamba moja nje kidogo ya mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.

Photo Credit
Viwavijeshi kwenye mashamba kusini mwa Afrika. Picha: FAO