Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR na wadau warejesha miundombinu ya umeme Iraq

UNHCR na wadau warejesha miundombinu ya umeme Iraq

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesaidia kurejeshwa kwa gridi ya umeme na miradi mingine ya usafi wa mazingira nchini Iraq, ikiwa ni miaka miwli toka kwa kuharibiwa kwa miundo mbinu hiyo kutokana na vita.

Hatua hiyo itasaidia maelfu ya familia mkoani Diyala nchini humo, hususani maeneo ambayo yalishilikiliwa na makundi ya waasi.

Taarifa ya UNHCR inasema kuwa shirika hilo kwa kuhsirikiana na asasi ya kiraia iitwayo YAO, wamerudisha umeme kwa kufunga transfoma 10 katika kila eneo, wakati serikali ya Iraq ilitoa ghrama za ufungaji na kuendesha mashine hizo.

Miradi hiyo iliwezeshwa kupitia ufadhili wa Euro 441,500 kutoka Serikali ya Italia.

Photo Credit
Picha: UN/Kibae Park