Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo bahari ya Mediterranean ni mara sita zaidi ya miezi 12 iliyopita: IOM

Vifo bahari ya Mediterranean ni mara sita zaidi ya miezi 12 iliyopita: IOM

Pakua

Takribani watu 365 hawajulikani walipo wakihofiwa kufa maji baada ya safari sita za kuvuka bahari ya Mediterranean kushia kwenye zahma wiki hii , limesema shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Kwa mujibu wa Leonard Doyle msemaji wa IOM idadi ya vifo kwenye bahari hiyo mwaka huu ni mara sita zaidi ya ilivyokuwa Novemba mwaka jana.

(SAUTI YA DOYLE)

"Hii bila shaka ni kutokana na hali mbaya ya hewa unafahamu, wahamiaji wanaanza safari na kulipia kwa matumaini kwamba watasafiri salama Mediterranean na kisha wanakuja ufukweni kukabiliana na zahima na hawana njia nyingine, wakati mwingine hata wanajizuia kimwili kwenda nyuma.”

Wahamiaji 4636 wamezama mwaka huu kwenye bahari hiyo ikiwa ni zaidi ya vifo 1000 ikilinganishwa na mwaka jana.

Photo Credit
Wakimbizi waliovuka bahari Mediterranean. (Picha:UNHCR/F.Malavolta)