Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yazindua video kabambe ya elimu ya jinsia

UNESCO yazindua video kabambe ya elimu ya jinsia

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO , limezindua video iitwayo “kuwa kijana”ambayo inaainisha jinsi gani elimu ya kina ya jinsia (CSE) inasaidia vijana ufahamu na ujusi wa kufanya uamuzi bora na uwajibikaji kuhusu mahuasiano na jinsia.

Kutolewa kwa video hiyo kunafuatia mkutano wa ngazi ya juu kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York uliokuwa na mada “kuboresha afya ya jinsia na uzazi kwa wasichana vigori: jukumu la wake wa Maraisi.

Kikao hilo kilichofanyika wiki iliyopita kimewaleta pamoja wa wakuu wa nchi na serikali, wake wa Maraisi, wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya asasi za kiraia, ili kuongeza kukubalika na uchukuaji wa hatua za kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi na jinsia kwa barubaru Afrika.

Akizungumzia suala hilo mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokoba amesema elimu ya afya ya uzazi na jinsia ni msingi kwa kuzuia maambukizi ya HIV na ni sehemu ya safari ya vijana kuelekea utu uzima. Ikiwa ni pamoja na kupunguza ndoa za utotoni na maambukizi ya maradhi kama ukimwi.

Photo Credit
UNESCO yandindua video kabambe ya elimu ya jinsia_Being a young person.Picha: World Bank/Allison Kwesell