Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha G20 kuunga mkono kusaini Mkataba wa Paris

Ban akaribisha G20 kuunga mkono kusaini Mkataba wa Paris

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amekaribisha leo taarifa kutoka kwa Urais wa nchi 20 tajiri zaidi duniani, G20, ambao unashikiliwa na Uchina, ikieleza uungaji mkono kikamilifu utiaji saini Mkataba wa Paris kuhusu tabianchi, ambao utafanyika katika hafla kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mnamo Aprili 22.

Aidha, Ban amekaribisha wito wa Urais wa G20 wa kutaka Mkataba huo wa Paris uanze kutekelezwa mapema iwezekanavyo.

Katibu Mkuu ameishukuru Uchina kwa uongozi wake imara katika kuchagiza ushirikiano wa kimataifa, kwa msingi wa hatua kabambe za kila taifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Ban ameeleza pia kutiwa moyo na msukumo thabiti wa kisiasa kutoka zaidi ya nchi 130 wanachama, ambazo zimethibitisha nia ya kutia saini Mkataba wa Paris mnamo tarehe 22 Aprili, 2016, na kutoa wito kwa nchi zingine kujiunga nazo kwenye hafla ya utiaji saini.

Photo Credit
katibu Mkuu Ban Ki-moon Picha ya UM/Jean-Marc Ferré