Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio la kigaidi Uturuki

Ban alaani shambulio la kigaidi Uturuki

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la kigaidi nchini Uturuki hii leo, shambulio linalodaiwa kuuwa watu kadhaa na kusababisha majeruhi.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu iliyotolewa leo mjini New York imesema kuwa shambulio hilo la bomu huko Uturuki kati , ni miongoni mwa mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

Ban katika taarifa hiyo ametaka watekelezaji wa ukatili huo aliouita wa kuogofya wafikishwe katika vyombo vya sheria kwa kuzingatia wajibu wa haki za binadamu.

Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio hilo na watu wa serikali ya Uturuki.

Photo Credit