Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© UNICEF/UN0560086/Gwenn Dubourthoumieu

Raia nchini DRC wasimulia jinsi wanavyonufaika na miradi iliyofanikishwa na MONUSCO

Kadri siku za MONUSCO kuondoka nchini DRC zinavyokaribia, vivyo hivyo wananchi wanufaika wa miradi iliyofanikishwa na ujumbe huo wanazidi kujitokeza kuelezea hisia zao, kwani ujumbe huo unatakiwa uwe umeondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.

Miongoni mwa wanufaika ni shule ya msingi Lubumba hapa Kamanyola na Mwalimu Mkuu Texas Chekabiri anaelezea hali ilivyokuwa. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuelezea zaidi katika makala hii.

Sauti
3'4"
Unsplash/Dan Meyers

UNICEF na jitihada za kuimarisha huduma za Afya ya Akili kwa vijana nchini Rwanda

Makala hii inaeleza safari ya matumaini na uthabiti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNICEF Rwanda linaposhirikiana na Rwanda Biomedical Center (shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya) kuleta mapinduzi katika huduma za afya ya akili kwa vijana. Katika mpango huu wa kutia moyo, UNICEF inavunja vizuizi na kukuza ujasiri kwa kutoa usaidizi muhimu kama vile nasaha shuleni

Sauti
2'54"
UNCTAD

UNCTAD, UNECA, Kenya kuunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia upatu lengo namba tano la Malengo Endelevu ya Umoja huo linalohimiza usawa kwa wote katika nyanja zote ifikapo mwaka 2030. Hata hivyo ili kuelewa jinsi biashara inavyoathiri wanaume na wanawake ni muhimu kuunda sera za biashara zinazojumuisha zaidi na zenye usawa ambazo zinakuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wote,hii inahitaji takwimu nzuri za kitaifa kuhusu jinsia katika biashara.

Sauti
3'8"
UNICEF VIDEO

Mradi wa maji warejesha matumaini kwa familia Wajir

Maji ni uhai, ni kauli mbiu ya miaka nenda rudi, lakini imesalia ndoto kwa wengi duniani hasa wakati huu mabadiliko ya tabianchi yanachochea ukame unaovuruga maisha ya binadamu, wanyama na mimea. Nchini Kenya katika kaunti ya Wajir, iliyoko kaskazini-mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, uhaba wa maji ulisababisha familia kupoteza mifugo yao, mazao kukauka na ustawi wa jamii kutoweka.

Sauti
4'24"