Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 JULAI 2024

22 JULAI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya juhudi za kutokomeza ukimwi, na miradi ya WFP kwa wakimbizi nchini Uganda. Makala tunamulika faida ngamia kkwa wafugaji nchini Kenya, na mashinani tunaangazia ziara za Fillipo Grandi nchini Ukraine.

  1. Ripoti mpya iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS na muungano  wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi unaojumuisha mashirika mbalimbali, inaonyesha kwamba dunia iko katika wakati muhimu wa kubaini endapo viongozi wa dunia watatimiza  ahadi zao  za      kumaliza janga la ukimwi kama tishio la afya ya umma  ifikapo mwaka 2030.
  2. Je wafahamu kuwa Uganda ndio nchi inayohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika? Na sera rafiki za maendeleo za nchi hiyo zinawapa wakimbizi fursa ya kuzalisha chakula chao wenyewe. Mmoja wa wanaofaidi sera hizo ni Jeniffer mkimbizi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC ambaye anaeleza ni muhimu kwa wakimbizi kuzalisha chakula chao wenyewe.
  3. Makala tunakwenda kauti ya Samburu Kaskazini mwa Kenya ambayo ni miongoni mwa maeneo mengi yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Jamii ya Wasamburu kwa kawaida ni wafugaji, baada ya ukame kukatili maisha ya mifugo yao haswa ng’ombe na mbuzi wakazi wengi walipoteza matumaini hadi pale FAO ilipowaletea mradi wa ufugaji wa ngamia kama mbadala wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
  4. Na mashinani tunamsikia Fillipo Grandi, Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambaye amehitimisha ziara yake mwishoni mwa wiki nchini Ukraine kushuhudia matokeo ya mlipuko wa hivi karibuni wa hospital ya Okhmatdyt.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
9'52"