Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 JULAI 2024

19 JULAI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia tishio la polio Gaza, na kauli za chuki zinazoweza kusababisha mauaji ya kimbari na ukosefu wa amani. Makala tunaangazia vijana kutoka Uganda katika mkutano wa HLPF hapa makao makuu, na mashinani tunakupeleka nchini Somalia, kulikoni?

  1. Wananchi wa Gaza wakikabiliwa na machungu ya kila namna, kugunduliwa kwa tishio la ugonjwa wa polio unaoambukiza sana unaohusishwa na hali mbaya ya usafi iliyosababishwa na mzozo unaoendelea kumekuwa kama kuongeza chumvi kwenye kidonda.
  2. Alice Wairimu Nderitu mashauri maalum wa Umoja wa Mataifa  katika kuzuia auaji ya kimbari akizungumza na UN New Kiswahili hivi karibuni na huku akitoa raia kuhusu mauaji hayo na kutaka kila mtu kumakinika na kuchukua hatua.
  3. Katika makala Anold Kayanda anazungumza na Monicah Malith mmoja wa vijana waliofika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria Jukwaa la Kisiasa la Ngazi za Juu la Umoja wa Mataifa (HLPF) mwaka 2024. Monicah Malith aliikimbia  nchi yake Sudan Kusini na kuingia Kenya.  Kupitia makala hii anaeleza kwa nini aliamua kuisoma kozi anayoisoma sasa katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwani ana matumaini kozi hiyo itasaidia kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.
  4. Na mashinani Fosiya Ibarahim Botan mkulima katika kijiji cha Erigavo nchini Somalia akitueleza jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, linasaidia wakulima kujikimu kimaisha kupitia msaada wa fedha taslimu, elimu na uundaji wa vyama vya mikopo vya akiba vya vijiji.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
9'57"