Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 JUNI 2024

21 JUNI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake huko Gaza, na masuala ya afya nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Ethiopia na mashinani tunasalia nchini Tanzania, kulikoni? 

  1. Baada ya ziara ya wiki moja huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, Maryse Guimond ambaye ni Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli,Israeli amesema kilicho alichoshuhudia hakina maelezo ya kutosha. 
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni (WHO) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), hivi karibuni limekabidhi kwa Wizara ya Afya nchini humo jengo maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wanaohisiwa kuwa na magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza wanapopita katika mpaka wa Mutukula unaounganisha Tanzania na Uganda kaskazini.
  3. Makala inatupeleka nchini Ethiopia ambako nchi hiyo kwasasa inatekeleza mpango wa kihistoria wa utoaji wa vitambulisho vya kitaifa unaojumuisha wakimbizi na wasaka hifadhi.
  4. Na mashinani tutakepeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe wa watoto kuhusu elimu.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
9'58"