Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaimarisha Afya ya Mifugo nchini Tanzania kupitia mradi wa ISAVET

FAO yaimarisha Afya ya Mifugo Kupitia mradi wa ISAVET Tanzania na Zanzibar Tanzania.
UN News
FAO yaimarisha Afya ya Mifugo Kupitia mradi wa ISAVET Tanzania na Zanzibar Tanzania.

FAO yaimarisha Afya ya Mifugo nchini Tanzania kupitia mradi wa ISAVET

Afya

Nchini Tanzania, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linaendesha programu ya mafunzo yanayolenga kuboresha ujuzi wa wataalamu wa mifugo katika kudhibiti magonjwa ya wanyama na kuimarisha afya ya mifugo ili kuihakikishia jamii uhakika wa chakula na chakula salama. 

Soundcloud

Programu ya mafunzo ya ISAVET (In-Service Applied Veterinary Epidemiology Training) inayofanikishwa na FAO nchini Tanzania inalenga kuboresha ujuzi wa wataalamu wa mifugo katika kudhibiti magonjwa ya wanyama na kuimarisha afya ya mifugo. Mafunzo haya yanahusisha wataalamu kutoka Tanzania bara na Zanzibar, na yanaendeshwa kwa ushirikiano wa karibu na serikali za maeneo haya mawili. 

ISAVET inalenga kuwapatia maafisa wa mifugo ujuzi wa kipekee wa utambuzi, ufuatiliaji, na udhibiti wa magonjwa ya mifugo. Programu hii ni muhimu kwa kuwa magonjwa ya mifugo yanaweza kuathiri sana uchumi na usalama wa chakula. Mafunzo yanajumuisha masomo ya darasani na mafunzo kwa vitendo ambapo washiriki wanajifunza mbinu bora za kuepuka na
kudhibiti milipuko ya magonjwa ya mifugo.

FAO yaimarisha Afya ya Mifugo Kupitia mradi wa ISAVET Tanzania na Zanzibar Tanzania.
UN News
FAO yaimarisha Afya ya Mifugo Kupitia mradi wa ISAVET Tanzania na Zanzibar Tanzania.

Kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar, FAO inahakikisha kuwa kuna ushirikiano mzuri kati ya pande zote mbili. Hii ni muhimu kwa kuwa ugonjwa unaweza kusambaa kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kujali mipaka ya kiutawala. Kwa hivyo, mafunzo haya yanaimarisha mfumo mzima wa afya ya mifugo nchini na kuleta uwiano katika jitihada za kudhibiti
magonjwa.

Kupitia ISAVET, FAO inachangia katika kuboresha maisha ya wafugaji na kuhakikisha kuwa sekta ya mifugo inakuwa na mchango mzuri katika uchumi wa Tanzania. Mafunzo haya pia yanahimiza ushirikiano wa kimataifa katika masuala ya afya ya wanyama, jambo ambalo ni muhimu katika dunia ya sasa yenye mwingiliano mkubwa.