Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi wa ADF waendelea kutesa raia Mashariki mwa DRC: MONUSCO

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu na MONUSCO wakishika doria karibu na mji wa Beni, Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
MONUSCO/Michael Ali
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu na MONUSCO wakishika doria karibu na mji wa Beni, Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Waasi wa ADF waendelea kutesa raia Mashariki mwa DRC: MONUSCO

Amani na Usalama

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO umesema kundi lenye silaha la waasi wa Allied Democratic Forces ADF wameendelea kuleta bughudha nje yam ji wa Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa kwa waandishi wa habari mjini New York Marekani leo, katika siku chache zilizopita kumekuwa na mshambulio kadhaa ya kundi hilo yaliyosababisha vifo vya raia.

Ili kukabiliana na mashambulizi hayo msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephanie Dujarric amesema “walinda amani wa Umoja wa Mataifa walipeleka askari kushika doria katika maeneo yaliyoathirika na wanaendelea kufuatilia kwa karibu hali inavyoendelea.”

Wakati huohuo katika jimbo la Kivu Kusini MONUSCO imefunga kituo chake cha Sange, kama sehemu ya utekelezaji wa makubaliano na serikali ya DRC wa kujiengua nchini humo.

Hata hivyo msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa MONUSCO itaendeleakutimiza wajibu wake wa kulinda raia katika jimbo la Kivu Kaskazini na Ituri lakini sio Kivu Kusini.