Hatua za kidiplomasia kusaidia DRC zakinzana na ukatili unaoendelea
Mikataba ya amani iliyofikiwa huko Washington nchini Marekani na Doha nchini Qatar ilileta matumaini ya hatua mpya katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Lakini wakati mawaziri wa mambo ya nje na wapatanishi wakiongeza idadi ya saini na mifumo ya ufuatiliaji, ghasia zinaendelea kumwaga damu katika maeneo ya Kivu Kaskazini na Ituri.