Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO Zambia, yashirikiana na Serikali kutokomeza Kipindupindu

Mtoto kutoka Mtedera Zambia akipweza chanjo ya kipindupindu.
Picha ya Gavi Alliance/Duncan Graham-Rowe
Mtoto kutoka Mtedera Zambia akipweza chanjo ya kipindupindu.

WHO Zambia, yashirikiana na Serikali kutokomeza Kipindupindu

Afya

Juhudi na ushirikiano wa pamoja wa wahudumu wa afya, vituo na Jamii, vimefanikisha kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia kwa mujibu wa Shirika Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO nchini Zambia, ambalo limeeleza kwamba ugunduzi wa mapema na matibabu husaidia kukabiliana na ugonjwa huo na kupunguza matukio na vifo.

Jioni moja Philta Samazimva alilalamika ghafla tumbo kuuma, baada ya kuharisha sana, mama yake mzazi Hildar Samazimba alimpeleka kliniki.

Baadhi ya watu hapa walisema usiende hospitali mtoto atapona, hakuna kitu watakachompatia mtoto na atakufa. Lakini nilipoona jinsi mtoto wangu alivyokuwa anaonekana, nilisema wacha niwahi kliniki.

Philta alipelekwa kwenye kituo cha matibabu cha Heroes Cholera, ambapo alipata ahueni  baada ya matibabu. Dr Mavis Chisala, Ni Daktari wa magonjwa ya watoto katika kituo cha kutibu kipindupindu cha Mashujaa. 

"Tumekuwa tukihakikisha tunamfuatilia mgonjwa wetu, kwa sababu kwa watoto wanaimarika haraka sana unapochukua hatua sahihi kwa wakati muafaka.

Kiwango cha vifo vya wagonjwa wa kipindupindu katika vituo vya afya ni asilimia 1.3, ikilinganishwa na asilimia 3.3 kwa ujumla, kutokana na kazi inayofanywa na matabibu hao kwa ushirikiano na WHO ambao umerejesha matumaini kwa Samazimba 

“ kikubwa tulifanya kazi kwa ushirikiano, ninawashukuru Wauguzi, matabibu kwa kazi waliyoifanya, kwasababu sikujua kama mtoto wangu atapona

WHO imeisaidia wizara ya afya nchini Zambia kurekebisha miongozo ya huduma za kliniki na kununua vifaa tiba na vifaa vingine kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu. Dkt. Kalima Nawa, kiongozi mkuu wa kituo cha matibabu cha mashujaa wa kipindupindu anasema Hold under……03 sec “tunatarajia kuendelea kufanya kazi na WHO katika mlipuko huu, na pia kupanga kwa ajili ya milipuko ya baadaye na kutusaidia kujiandaa kwa hayo”.

Kipindupindu kinatibika kwa urahisi iwapo kitagunduliwa kwa wakati.