Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNRWA aonya hali mbaya zaidi yaja Gaza licha ya jinamizi linalowaghubika sasa

Kamishina Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini akizungumza katika mkutano usio rasmi wa Baraza Kuu kuhusu UNRWA
UN Photo/Evan Schneider
Kamishina Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini akizungumza katika mkutano usio rasmi wa Baraza Kuu kuhusu UNRWA

Mkuu wa UNRWA aonya hali mbaya zaidi yaja Gaza licha ya jinamizi linalowaghubika sasa

Amani na Usalama

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Philippe Lazzarini amesema asilimia 5 ya wakazi wa Gaza ama wameuawa, kujeruhiwa au kupoteza mwelekeo wao. 

Amesema “mateso yanayowakabili watu katika Ukanda huo hayawezi kuelezewa vya kutosha, kwani madaktari wanalazimika kukata viungo vya watoto waliojeruhiwa bila ganzi, njaa inatapakaa kila kona , na baa la njaa inayosababishwa na wanadamu linajongea.”

Katika mkutano uliofanyika kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo mjini New York kuhusu kazi za UNRWA, Lazzarini ameeleza kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa siku chache zilizopita walipokuwa wakitafuta chakula, huku watoto wakiwa wamepoteza maisha mchanga akiwa na umri wa miezi michache tu amekufa kwa utapiamlo na upungufu wa maji mwilini.

Lazzarini  ameongeza kuwa "Ninatetemeka ninapofikiria juu ya maafa yatakayoibuka katika ukanda huu mwembamba wa ardhi. Je, nini kitatokea kwa watu wapatao 300,000 waliotengwa kaskazini mwa nchi, ambao wametengwa na misaada ya kibinadamu? Ni watu wangapi ambao bado wako chini ya vifusi. Ukanda wa Gaza? Nini kitatokea? watoto wapatao 17,000 watakapokuwa mayatima, walioachwa katika eneo lenye hatari zaidi na lisilo na sheria.”

Lazzarini amesema shambulio la Rafah ambako takriban watu milioni 1.4 waliokimbia makazi yao wamejrundikana liko karibu. 

Amesisitiza kuwa hakuna mahali salama pa wao kwenda akiongeza kuwa "Licha ya maovu yote ambayo watu wa Gaza wamepitia na ambayo tumeshuhudia mbaya zaidi yanaweza kuwa bado yanakuja."

Zaidi ya shule 80 za UNRWA zimeshambuliwa au kubomolewa kwa makombora tangu kuanza kwa mzozo wa karibuni Gaza
© UNRWA
Zaidi ya shule 80 za UNRWA zimeshambuliwa au kubomolewa kwa makombora tangu kuanza kwa mzozo wa karibuni Gaza

Amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki

Lazzarini amedokeza kuwa Januari 26, Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, ilitoa amri ya kisheria yenye hatua za muda zinazohusiana na Wapalestina huko Gaza, ikiwa ni pamoja na kuitaka Israel kuchukua hatua zote ndani ya uwezo wake ili kuzuia kufanyika kwa vitendo ambavyo viko ndani ya wigo wa Kifungu cha II cha Mkataba wa Mauaji ya Kimbari.

Amesema hii ni pamoja na kuwezesha utoaji wa huduma za msingi zinazohitajika na misaada. 

Ameongeza kuwa agizo hili lilitolewa katika mazingira ya vita, ambapo miezi mitano pekee ilisababisha mauaji ya watoto, waandishi wa habari, wahudumu wa afya na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, kwa idadi kubwa kuliko sehemu nyingine yoyote duniani wakati wa migogoro.

Watoto wakimbizi wa ndani wakiwa kwenye makazi yamjini Rafah Kusini mwa Gaza
© WHO
Watoto wakimbizi wa ndani wakiwa kwenye makazi yamjini Rafah Kusini mwa Gaza

Madai, uchunguzi wa haraka na tathimini huru

Lazzarini amesema kuwa mamlaka ya Israel ilimwambia wiki moja kabla ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kutoa uamuzi kwamba "wafanyakazi 12 kati ya 30,000 wa UNRWA wanadaiwa kushiriki katika mashambulizi ya kutisha ya Oktoba 7 mwaka jana." 

Ameongeza kuwa tangu siku hiyo hajapata taarifa zaidi kuhusiana na suala hilo, lakini uzito wa tuhuma hizo unamtaka achukuwe hatua za haraka na kusitisha mikataba ya watumishi husika kwa manufaa ya shirika hilo.

Ameelezea maendeleo ya michakato miwili sambamba kwanza uchunguzi huru uliofanywa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma za Uangalizi wa Ndani ili kufichua ukweli kuhusu madai haya, na pili tathimini huru ya kando iliyoagizwa na Katibu Mkuu ya mbinu ya UNRWA ya kushughulikia usimamizi wa masuala ya hatari na kutoegemea upande wowote.

Licha ya hatua za dharura na madhubuti na hali isiyothibitishwa ya madai hayo, Lazzarini amesema, nchi 16 zilisitisha ufadhili wao kwa UNRWA, ambao ni jumla ya dola milioni 450. 

Kamishna Mkuu ameonya kwamba UNRWA haiwezi kukabiliana na janga la kifedha haswa kwa kutilia maanani kuendelea kwa vita huko Gaza.

Kwa kuzingatia changamoto ambazo zimeifikisha UNRWA kwenye "ukingo wa kuporomoka," Kamishna Mkuu Philippe Lazzarini, amesisitiza mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa haja ya kutatua mzozo wa kifedha unaolikabili shirika hilo ili liweze kuendelea operesheni zake za kuokoa maisha ya watu.