Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukraine: Bucha na Irpin zinaibuka kutoka kwenye majivu ya uvamizi wa jeshi la Urusi

Kitongoji hiki huko Bucha kiliteseka sana wakati wa uvamizi wa Urusi. Nyumba hii ilipigwa bomu. Leo kila kitu kimerejeshwa kabisa.
UN News/Anna Radomska
Kitongoji hiki huko Bucha kiliteseka sana wakati wa uvamizi wa Urusi. Nyumba hii ilipigwa bomu. Leo kila kitu kimerejeshwa kabisa.

Ukraine: Bucha na Irpin zinaibuka kutoka kwenye majivu ya uvamizi wa jeshi la Urusi

Amani na Usalama

Wakati uvamizi wa Urusi huko Bucha katika siku za mwanzo za uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine, ulimalizika mnamo Machi 2022, uharibifu mkubwa ulionekana, na tume ya Umoja wa Mataifa ikihitimisha kwamba uhalifu wa kivita ulikuwa umetendwa dhidi ya raia, miaka miwili baadaye, maisha yanarudi katika mji ulio nje kidogo ya Kyiv, ambao umerejeshwa kwa msaada wa UN.

“Walikuwa wanaruka na helikopta kutoka upande wa uwanja wa ndege wa mizigo huko Hostomel kaskazini mwa Bucha, kisha wakaendelea na mizinga kando ya Mtaa wa Vokzalna, wakavuka reli na kuelekea Kyiv," anasema Mykhaylina Skoryk Shkarivska, mwanzilishi wa Taasisi ya Maendeleo Endelevu ya Jamii huko Bucha na naibu wa Halmashauri ya Jiji la Irpin, akikumbuka siku za kwanza za uvamizi wa jeshi la Urusi. 

Uvamizi wa wanajeshi wa Urusi ulidumu karibu mwezi mzima na wakati jiji lilikombolewa mnamo Machi 31, 2022, ushahidi wa mauaji, mateso na uhalifu mwingine uliofanywa na jeshi la Urusi, pamoja na uharibifu mwingi, ulionekana.

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk akiwa mji mkuu wa Ukraine Kyiv mwanzoni mwa ziara rasmi nchini humo, mwaka 2022. (Maktaba)
OHCHR
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk akiwa mji mkuu wa Ukraine Kyiv mwanzoni mwa ziara rasmi nchini humo, mwaka 2022. (Maktaba)

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Türk, akizuru jiji hilo mwezi Desemba 2022, alisema kuwa ilikuwa vigumu kwake kufikiria juu ya yale ambayo wakazi wa Bucha walipaswa kupitia.

“Unasikia kuhusu askari wanaokuja kijijini kwako au mji wako, halafu unaona askari hao, unaona wanaanza kuua watu mitaani, kisha risasi za sniper, risasi, mauaji ya watu wengi, mauaji ya muhtasari."

Ripoti ya Umoja wa Mataifa juu ya ufuatiliaji waMisheni nchini Ukraine inarejelea mauaji yaliyorekodiwa ya wakaazi wa eneo hilo, jeshi la Urusi, kulingana na waandishi wa ripoti hiyo, mara nyingi walifanya mauaji ya katika vituo vya ukaguzi: ujumbe wa maandishi kwenye simu, kipande cha sare ya kijeshi au cheti cha utumishi wa kijeshi hapo awali inaweza kusababisha matokeo mabaya.

Mnamo Septemba 2022, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Karim Khan, alizungumza na wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu matokeo ya uvamizi huo. 

"Katika jiji la Bucha, nilitembelea Kanisa la Mtakatifu Andrew, ambapo niliona miili iliyofichwa nyuma ya jengo, hii sio udanganyifu, nilipokuwa nikipita kwenye mitaa ya Borodyanka, niliona shule na nyumba zilizoharibiwa, hii ni kweli, uharibifu, niliuona," alisema wakati huo imekadiriwa kuwa maelfu ya majengo huko Bucha yaliharibiwa na zaidi ya mia moja kuharibiwa kabisa.

Mtaa wa Vokzalnaya huko Bucha leo. Sekta ya nyumba ya kibinafsi, ambayo ilikuwa imeharibiwa vibaya, imerejeshwa kikamilifu.
UN News/Anna Radomska
Mtaa wa Vokzalnaya huko Bucha leo. Sekta ya nyumba ya kibinafsi, ambayo ilikuwa imeharibiwa vibaya, imerejeshwa kikamilifu.

Kuirudisha Bucha kwenye uhai

Lakini leo, karibu miaka miwili baada ya uvamizi, kuna ishara za kushangaza za uamsho, Umoja wa Mataifa umefanya kazi kwa karibu na mamlaka za mitaa, serikali na washirika wa kimataifa, ili kuhakikisha jiji hilo linaweza kuwa hai haraka iwezekanavyo, "katika robo ya Nova Bucha kila kitu kiliharibiwa wakati wa uvamizi, sasa imekuwa karibu kabisa kujengwa, "anasema Bi. Skoryk-Shkarivska.

"Majengo yote ya ghorofa yaliyoharibiwa yanafanyiwa ukarabati kwa njia thabiti, paa zinabadilishwa kabisa, umeme wa joto umewekwa, ili jengo liweze kuhifadhi joto vizuri zaidi, ni ngumu kuamini kwamba miaka miwili iliyopita kulikuwa na msafara wa vifaa vya kijeshi vya Urusi hapa, na karibu nyumba nyingi zilikuwa zimevunjwa au kuchomwa moto”.

"Wakati mwingine nasikia majadiliano juu ya ikiwa ni muhimu kujenga upya, lakini eneo la Kyiv haupati mashambulizi makubwa ya Urusi, kwa mfano, maeneo ya mpaka wa mkoa wa Kharkiv, watu wanarudi, wanahitaji kuishi na kufanya kazii, jiji linaishi, kuna biashara, kuna migahawa mingi mpya, jiji lililo hai linahitaji kujengwa upya, na kisha watu wengi zaidi watakuja, baada ya yote, mikoa ya magharibi ya Ukraine, ambapo kila mtu alikimbia mwanzoni, wamejaa kupita kiasi, hakuna cha kufanya kwa raia wengi huko hapa Kyiv, kuna kazi nyingi, fursa nyingi zaidi”.

Makazi katika shule huko Irpin, iliyokarabatiwa na UNICEF.
UN News/Anna Radomska
Makazi katika shule huko Irpin, iliyokarabatiwa na UNICEF.

Ukarabati wa hifadhi ya nyumba unasaidiwa na kufadhiliwa na washirika wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ambayo pia yanajishughulisha na kusafisha vifusi na uchimbaji wa madini katika eneo la Kyiv, hasa huko Bucha. 

Shule ya Irpin, ambayo ilikuwa kitovu cha mapigano makali mwaka 2022, sasa imerejeshwa kikamilifu na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), na leo ni mojawapo ya taasisi za kisasa zaidi za elimu mjini humo, ikiwa na makao yenye vifaa vya kutosha. na nafasi inayojumuisha.

"Mara tu Bucha na Irpin katika mkoa wa Kyiv waliporejea kwenye udhibiti wa serikali, UNICEF ilianza mipango ya ukarabati na kutoa msaada wa kina," anaelezea Munir Mammadzadeh, Mwakilishi wa UNICEF nchini Ukraine. 

"Zaidi ya watoto 5,000 huko Bucha na Irpin wanasoma katika shule zilizojengwa upya, ikijumuisha shule ya Irpin, ambayo asilimia 70 iliharibiwa na kurejeshwa kwake kulifadhiliwa na Muungano wa Ulaya (EU), sasa shule hii inafanya kazi kikamilifu na inatoa elimu ya wakati wote kwa wanafunzi 1,700, ikiwa ni pamoja na watoto wa watu waliohamishwa, na kuwapatia elimu kamili."

"Kwa watoto wengi, nchini Ukrainia na nje ya nchi, vita vimechukua miaka miwili ya shule, wakati wa kucheza na marafiki na fursa ya kuwasiliana na wapendwa wao, iliwanyima elimu, furaha na utoto wa kawaida, imekuwa na athari mbaya kwa afya yao ya akili”

“Tunahitaji kupunguza hasara za elimu. Walimu wa shule ya chekechea ambao sasa wamepewa mafunzo ya kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto, wana uwezo bora zaidi, kuwaunga mkono katika kipindi kigumu kama hiki."