Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuita vita ya Ukraine mgogoro ni kuidunisha ikilinganishwa na hali halisi ya kila siku: Mratibu Mkazi wa UN

Uharibifu wa majengo na miundombinu nchini Ukraine umesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
UNOCHA/Serhii Korovayny
Uharibifu wa majengo na miundombinu nchini Ukraine umesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

Kuita vita ya Ukraine mgogoro ni kuidunisha ikilinganishwa na hali halisi ya kila siku: Mratibu Mkazi wa UN

Amani na Usalama

Leo Februari 24, 2023 ni mwaka mmoja tangu uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine. 

Leo Februari 24, 2023 ni mwaka mmoja tangu uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine. 

Watu wa Ukraine wanaendelea kuwa wastahimilivu na wenye mnepo mwaka mmoja tangu uvamizi huo lakini "msaada wa kibinadamu ni muhimu kama ilivyokuwa zamani, kulingana na afisa wa Umoja wa Mataifa nchini humo. 

Denise Brown ni mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na wa misaada ya kibinadamu nchini Ukraine. 

Akiwa katika mji mkuu wa Kyiv, anafanya kazi pamoja na mashirika 20 ya Umoja wa Mataifa yenye takriban wafanyakazi 2,600, wengi wao wakiwa Waukrani. 

Amezungumza na UN News kuhusu changamoto za kusaidia jamii katika nchi iliyo kwenye vita. 

"Hali imekuwa ngumu sana nchini Ukraine katika mwaka uliopita na tumelazimika kuzoea hali zingine mbaya. Kuna ving'ora vya mara kwa mara vya uvamizi wa anga, ambayo vinamaanisha tunaingia na kutoka nje ya handaki siku nzima. Katika miezi 12 iliyopita tumehesabu kuwa tumetumia zaidi ya mwezi mmoja huko kufanya mikutano ya aina zote, ikijumuisha na timu ya kitaifa ya masuala ya Kibinadamu au nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.” 

Mratibu Mkazi na Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Denise Brown akikutana na wakazi wawili wa mji wa mstari wa mbele wa Mykolayiv, kusini mwa Ukraine.
UNOCHA/Saviano Abreu
Mratibu Mkazi na Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Denise Brown akikutana na wakazi wawili wa mji wa mstari wa mbele wa Mykolayiv, kusini mwa Ukraine.

Kusaidia watu wa Ukraine 

Mratibu huyo anasema siku zetu hapa mara nyingi hazitabiriki. Hakuna siku ya kawaida, lakini moja ninayokumbuka sana ilikuwa tarehe 10 Oktoba wakati kituo cha Kyiv kilipopigwa na mashambulizi ya anga saa 2.20 asubuhi kilomita 1.2 tu kutoka ofisi yangu.  

Niliposikia mlipuko huo na ofisi ikaanza kutetemeka, nilifikiri "oh sasa ungekuwa wakati mzuri wa kuingia kwenye chumba hicho cha kulala. 

Lengo letu kuu ni kusaidia watu wa Ukraine hasa kwa utoaji wa vifaa vya misaada. Tunafanya kazi karibu iwezekanavyo na mstari wa mbele, hali ambayo inahitaji mipango na uratibu wa kina. 

Mimi hutembelea jamii zilizo mstari wa mbele mara kwa mara kwa sababu ninasisitiza kwamba wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanahusika katika utoaji huu mgumu zaidi wa misaada.  

Tuna uwezo, uzoefu na rasilimali. Kwa hivyo, tunatumia muda kidogo sana katika maeneo kama Kherson, lakini pia katika jamii mbalimbali za mikoa ya Kharkiv, Zaporizhzhia na Donetsk. 

Mwezi Novemba, kulikuwa na tumaini kama hilo wakati mji wa Kherson ulipochukuliwa tena na Serikali ya Ukraine.  

“Siku tatu baadaye, tulikuwa huko na hali ilikuwa ya kusisimua sana. Kulikuwa na watu mitaani, wakitupungia mkono tulipoingia jijini na lori zilizojaa msaada. Lakini miezi kadhaa baadaye, kama ulivyoona wiki iliyopita, kulikuwa na kuendelea kwa mashambulizi ya anga katikati ya jiji na raia waliuawa, wafanyakazi wa kujitolea wameuawa, wafanyakazi wa misaada wamejeruhiwa. unahisi kama hali hii haitaisha kwa Kherson.” 

Lakini pia, kisichoishia kwa Kherson ni mnepo na matumaini ya watu waliobaki pale na ambao wameniambia hawataondoka. Huu ni ushuhuda wa kweli wa nguvu, imani na ujasiri wa idadi kubwa ya watu wa Ukraine. 

Watoto wakicheza mpira wa kikapu katika shule moja mjini Kharkiv iliyoharibiwa mwanzoni mwa vita. Shule bado haijajengwa upya, lakini watoto wanaweza angalau kurejesha hali ya kawaida kwa kucheza nje pamoja.
© UNICEF/Mykola Synelnykov
Watoto wakicheza mpira wa kikapu katika shule moja mjini Kharkiv iliyoharibiwa mwanzoni mwa vita. Shule bado haijajengwa upya, lakini watoto wanaweza angalau kurejesha hali ya kawaida kwa kucheza nje pamoja.

Kuzijenga upya jamii 

Mwezi Januari nilisafiri hadi karibu na Soledar, na kando ya barabara niliona jumii zilizokuwa zimetawanywa kabisa.  

Nina hakika kwamba uamuzi wa watu wa Ukraine utamaanisha kuwa miji na jamii hizi zitajengwa upya ingawa inaweza kuchukua muda mrefu.  

“Ujasiri na dhamira ya kufanya hivyo imeenea sana hapa. Ni jambo ambalo linanigusa katika maeneo yote ninayotembelea.” 

Tangu nilipowasili, nimetenga muda wa kuzungumza na watu katika jamii ninazotembelea, kukutana na kuzungumza na wafanyakazi wa kujitolea, mamlaka za mitaa, na mameya.  

Nadhani labda kuna watu wawili, wote wanawake, ambao nawakumbuka sana, mameya wa Kherson na Orikhiv, ambayo iko umbali wa kilomita tatu kutoka mstari wa mbele wamapambano, katika mkoa wa Zaporizhzhia.  

Nilikuwa hapo kwa chini ya saa tatu na tulihesabu angalau mashambulizi, 20 mahali pote kutoka umbali wa kilomita tano hadi 10. Ni milipuko tu ya mara kwa mara. 

Mameya hawa wameamua kubaki na wanafanya kazi bila kukoma, wakitunza jamii zao na ndio watendaji wetu wa msingi ambao tunawasiliana nao mara kwa mara. 

Wakati wa safari hiyo kwa jamii zilizo karibu na Soledar pia nilikutana na mwanamke mzuri sana, daktari.  

“Alinipeleka kwenye zahanati ambayo alilazimika kuanzisha nyumbani kwake baada ya kituo cha afya cha kijiji hicho kushambuliwa. Aliniambia jinsi alivyodhamiria kubaki hapo na kuwaunga mkono watu waliobaki nyuma. 

Kwa hiyo, hawa ni wanawake jasiri ambao nadhani sitawasahau kamwe.” 

Mahitaji ya kibinadamu 

Vita inaendelea na inaongezeka, kwa hivyo tunaweza kutarajia kwamba idadi ya watu itaendelea kuathiriwa.  

Huu ni mzozo wa kibinadamu, ingawa kuuita janga unaonekana kuwa duni sana ikilinganishwa na hali halisi ya kila siku tunayoiona. 

Hakuna hitaji moja kuu lakini mengi. Hali mbaya zaidi iko karibu na mstari wa mbele, ambako nyumba zimesambaratishwa na vituo vya afya vinaharibiwa. Kliniki moja niliyotembelea katika eneo la Kharkiv iliharibiwa mwezi mmoja baada ya kuitembelea. 

Jamii hizi zinahitaji kila kitu, kwa hivyo tumejitolea sana kuwasilisha bidhaa za msaada. 

 Pia tunaangazia sana kiwewe cha kisaikolojia wanachopata hasa watoto lakini kuwatunza kunazidi kuwa vigumu kadiri tunavyokaribia mstari wa mbele. 

Wafanyakazi wa kujitolea wakigawa chakula moto kwa watu waliopoteza makazi yao kutokana na tetemeko la ardhi huko Türkiye.
© UNOCHA/Matteo Minasi
Wafanyakazi wa kujitolea wakigawa chakula moto kwa watu waliopoteza makazi yao kutokana na tetemeko la ardhi huko Türkiye.

Katika mstari wa mbele wa mapambano 

Tuna fursa ya kufikia maeneo yote yanayodhibitiwa na Ukraine, lakini hatua fursa  sana ya kufika katika mstari wa mbele wa mapambano.  

Tangu Februari 2022, hakuna misafara ya kibinadamu iliyoweza kuvuka kati ya maeneo hayo mawili.  

Tunaomba fursa ya kuweza kufika huko mara kwa mara katika wizara za ulinzi nchini Ukraine na Urusi, na ingawa tunapokea jibu chanya kila mara kutoka kwa upande wa Ukraine, bado hatujapokea jibu kama hilo kutoka Urusi. 

Ni muhimu tuwe na fursa ya kufika katika mstari huo wa mbele. Tutaweza kwenda kesho ikiwa tutapata ruhusa lakini hakikisho la usalama linahitajika.  

“Ni muhimu, na ni muhimu sana kutuma vifaa na kusaidia watu wanaoishi ng'ambo ya mstari wa mbele, ambao nina hakika wako katika hali ya kukata tamaa. 

Mateso yanaendelea na hadi vita iishe, tunapaswa kuendelea kusaidia watu wa Ukraine, ambao wanaishi katika hali ya kutisha inayosababishwa na uvamizi huu wa Urusi." 

Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa 

• Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, wakati mwingine huitwa RC, ndiye mwakilishi wa ngazi ya juu zaidi wa mfumo wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa katika ngazi ya nchi. 

• Katika mfululizo huu wa mara kwa mara, UN News inawaalika RCs kuelezea na kuandika kuhusu masuala muhimu kwa Umoja wa Mataifa na nchi wanamohudumu.