Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza Kuu atoa wito wa mshikamano na Ukraine huku vita visivyo na maana vikiingia mwaka wa tatu

Majengo yaliyoharibiwa katika kijiji cha Borodyanka katika jimbo la  Kiev Ukraine
UN News/Аnna Radomska
Majengo yaliyoharibiwa katika kijiji cha Borodyanka katika jimbo la Kiev Ukraine

Rais wa Baraza Kuu atoa wito wa mshikamano na Ukraine huku vita visivyo na maana vikiingia mwaka wa tatu

Amani na Usalama

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis amezitaka nchi kusimama na watu wa Ukraine "katika harakati zao za kutafuta haki na amani" wakati wa mkutano uliofanyika leo Kwenye Baraza Kuu jijini New York kuadhimisha miaka miwili ya uvamizi kamili wa Urusi nchini humo.

Bwana Frabcis amesema "Tunapotafakari miaka miwili ya dhiki na shida, hebu tutoke mahali hapa tukiwa na ujumbe mzito wa mshikamano na uungwaji mkono usioyumbayumba kwa watu wenye wa Ukraine wenye mnepo wa hali ya juu." 

Baraza la Usalama pia linatazamiwa kukutana baadaye leo kuhusu Ukraine, ambapo mashambulizi mapya yameripotiwa katika miji ya Odesa na Dnipro, siku moja tu baada ya mashambulizi mabaya katika eneo la Donetsk, lililoko mashariki.

Uharibifu na athari

Akiwahutubia wawakilishi wa nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa waliokusanyika katika Ukumbi wa Baraza Kuu Bwana. Francis amesema "hawawezi kupofua macho uharibifu na uharibifu unaoendelea, wala kupuuza masaibu ya watu wa Ukraine."

"Hii ni muhimu hasa kwa sababu mwaka huu pia unaambatana na kumbukumbu ya miaka kumi ya jaribio Shirikisho la Urusi, la 2014 la kunyakua Crimea na maeneo mengine ya Ukraine.”

Uvamizi kamili wa Urusi ulianza tarehe 24 Februari 2022. Maelfu ya watu wameuawa na kujeruhiwa, mamilioni zaidi kutawanywa, na shule, hospitali na miundombinu mingine muhimu kuharibiwa. Watoto wengi wa Ukraine pia wamefukuzwa kutoka nchini Urusi kwa lazima.

Familia ikipatiwa huduma ya matibabu Odesa baada kukimbilia Kherson Ukraine
© UNICEF
Familia ikipatiwa huduma ya matibabu Odesa baada kukimbilia Kherson Ukraine

Athari kubwa duniani kote

Rais huyo wa Baraza Kuu Francis amesema athari za "vita visivyo na ulazima zimeenea zaidi ya mipaka ya Ukraine kwani mazingira pia ni mwathirika wa kimyakimya wa mzozo, wakati hatari halisi ya ajali ya nyuklia inaendelea. Na, hatimaye, vita vimeathiri kila nchi mwanachama aliyekusanyika katika ukumbi huu iwe kwa njia ya kupanda kwa bei ya vyakula au katika muktadha wa uhaba wa nishati."

Zaidi ya hayo, amesema mzozo huo umekuwa kichocheo kikubwa katika kuunda upya siasa za jiografia na uchumi wa kijiografia, kwani unadhuru moja kwa moja nchi zinazohusika huku pia ukizuia maendeleo katika zingine nyingi, haswa mataifa yanayoendelea.

Katiba ya Umoja wa Mataifa imedhoofishwa

Ameongeza kuwa vita hiyo "Inadhoofisha kikamilifu misingi ya katiba yetu ya Umoja wa Mataif, inatishia kanuni za uhuru, na uadilifu wa eneo ambalo sote tulijitolea kuheshimu na kutetea".

Ameendelea kusema kwamba pia "Imevuruga uwiano dhaifu wa mahusiano ya kimataifa wakati ambapo umoja, mshikamano na ushirikiano ni muhimu kabisa katika utatuzi wa changamoto za kimataifa”.

Bwana Francis amebainisha kuwa wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15 limelemazwa na mgawanyiko kuhusu mzozo huo, Baraza Kuu limelaani uchokozi wa Urusi na kutaka kuondolewa mara moja, kikamilifu na bila masharti kwa vikosi vyake kutoka ardhi ya Ukraine.

Vita nchini Ukraine imeleta athari kubwa kwa watoto
© UNICEF/Aleksey Filippov

Kuifanyia kazi amani

Amehitimisha tarifa yake kwa kusema kwamba "Zaidi ya kulaaniwa, sisi, Umoja wa Mataifa, lazima tufanye kazi kikamilifu kuelekea amani ya kudumu ya haki na endelevu kulingana na katiba ya shirika hili," 

Rais huyo wa Baraza Kuu ametoa wito wa kuongeza juhudi "kukomesha vita na kuleta mustakabali wa matumaini, ahadi na ustawi kwa watu wa Ukraine na Urusi, kwa usawa wa kweli na mahali popote, bila ubaguzi."