Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uondoaji wa mabomu ya kutengwa ardhini Ukraine ni mtihani na hatari kubwa: Paul Heslop

UNDP inasaidia kutegua mabomu ya ardhini nchini Ukraine.
UNDP in Ukraine/Alexander Ratushnyak
UNDP inasaidia kutegua mabomu ya ardhini nchini Ukraine.

Uondoaji wa mabomu ya kutengwa ardhini Ukraine ni mtihani na hatari kubwa: Paul Heslop

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa umesema Ukraine sasa ni moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na mabomu ya kutegwa ardhini duniani huku ikadiriwa kwamba karibu thuluthi moja ya nchi hiyo imeghubikwa na vita eneo ambalo ukubwa wake ni mara nne na nusu ya nchi ya Uswisi. Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kazi na serikali ya Ukraine kwa miaka 30 na umekuwa ukiongoza mpango wa utekelezaji wa uteguaji wa mabomu ya kutegwa ardhini tangu 2016. 

Paul Heslop Mshauri Mkuu wa Kiufundi wa utekelezaji wa program ya hatua ya uteguaji mabomu ya kutegwa ardhini ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Ukraine akisema amekuwa akifanya kazi ya uteguzi wa mabomu ya kutegwa ardhini kwa miaka thelathini katika maeneo hatari yenye vita, kuanzia Msumbiji hadi Afghanistan. Lakini aliyoyashuhudia ilikuwa maandalizi tu mtihani kamili ambao sasa uko Ukraine.

“Ni mazingira magumu sana iwe ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiufundi, kwanza kabisa kwa maana ya kieneo, ni nchi kubwa. Kuna mstari wa mbele wa vita ambao sasa ni zaidi ya kilomita elfu moja, kuna uwezekano wa kazi kubwa ya kufanya. theluthi moja ya nchi inashukiwa kuathirika na mabomu ya ardhini. Hiyo ni ukubwa wa kama nchi mbili za Ufaransa.”

Mathalani Paul anasema, 

“Endapo makombora 30,000 yanarushwa kwa siku, hayo ni mabomu 3,000 yasiyolipuka kwa siku. Na, wakati mzozo unafikia siku elfu moja basi, hayo ni mabomu milioni 3 na vilipuzi vingine ambayo hviajalipuka.”

Licha a hali kuonekana ni ya kutisha lakini haimkatishi tamaa  Paul wala kumfanya ajutie kufanyakazi ya ya Umoja wa Mataifa ya uteguzi mabomu.. 

“Nimebaini kwamba kufanya kazi kya kutegua mabomu kuwa ni kazi bora zaidi ambayo ningeweza kuwa nayo. Nimeona ushujaa ambao siwezi hata kuamini na nimeshuhudia matukio ambayo yananitia hofu kubwa.”

Kwa mujibu wa UNDP ambayo ni mratibu wa hatua za kutegua mabomu ya ardhini Ukraine hadi kufikia Juni mwaka huu mabomu na vilipuzi 540,000 ambavyo havikulipuka vimeteguliwa, lakini kuifanya Ukraine kuwa salama kabisa ni kibarua kigumu na cha gharama kubwa, huku Benk ya dunia ikikadiria kuwa kutegua vilipuzi na mabomu yote nchini humo kutagharimu dola  zaidi ya bilioni