Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yaafikiana na serikali ya DRC mikakati ya kuondoka nchini humo

Bi. Keita akizungumza na wanahabari huko Kalehe, Kivu Kusini.
MONUSCO/Michael Ali
Bi. Keita akizungumza na wanahabari huko Kalehe, Kivu Kusini.

MONUSCO yaafikiana na serikali ya DRC mikakati ya kuondoka nchini humo

Amani na Usalama

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Mkuu wa wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSC, Bi Bintou Keita na Naibu Waziri Mkuu, na Waziri wa Mambo ya nje Francophonie Christophe Lutundula walithibitisha jana Jumamosi Januari 13, dhamira ya vyombo hivyo viwili kufanya kazi kwa pamoja kwa mchakato wa kuondoka kwa MONUSCO nchini DRC kwa njia ya maendeleo, kuwajibika, heshima na kwa MONUSCO kuwa mfano wa kuigwa. 

Viongozi hao wameyasema hayo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari mjini Kinshasa.

MONUSCO imesema “Utengano huu utafanywa kwa awamu tatu tofauti, kulingana na mpango uliosainiwa Novemba 21 na Bi Keita naBwana. Lutundula. Timu zetu zilifanya kazi katika umoja, kwa rmoyo wa kujenga na kwa hisia kubwa ya uwajibikaji.”

Wameainisha mchakato huo wa kujiengua kwa MONUSCO na kuweka masharti ya uhamishaji wa taratibu wa majukumu kutoka MONUSCO kwenda kwa serikali ya Congo. 

Baraza la Usalama limeidhinisha mpango huu na kwa pamoja tutatumia mkakati huu wa kujiengua ili kubadilisha maono ya mkuu wa nchi ili kufanya uondokaji wa MONUSCO kuwa mfano wa mabadiliko ya operesheni ya amani ya Umoja wa Mataifa alisema Christophe Lutundula.

Ni wakati wa kihistoria

Kwa upande wake, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo DRC, Bi Bintou Keita, amewashukuru viongozi wa Congo kwa kujitolea kwao na kushirikiana kwa uwazi katika mchakato wote.

"Kwa mara ya kwanza, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linachukua jukumu la wito kwa MONUSCO kuanza kujiondoa kutoka DRC. Huu ni wakati wa kihistoria. Tutafanya juhudi yoyote na wenzetu wa Congo kukamilisha mchakato huu kwa mafanikio.”

Ameongeza kuwa “Ninakaribisha hamu ya viongozi wa Congo kufanya kuondoka kwa MONUSCO kuwa mfano wa mabadiliko ya mafanikio ya operesheni za kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.”

Bintou Keita, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO), akihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchini DRC.
UN Photo/Cia Pak
Bintou Keita, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO), akihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchini DRC.

Awamu tatu za kuondoka kwa MONUSCO DRC

Viongozi hao wameweka bayana kwamba mchakato huu wa MONUSCO kuondoka DRC utafanyika katika awamu tatu tofauti.

Awamu ya kwanza ya mpango huu inahusu uondoaji kamili wa jeshi na polisi wa MONUSCO kutoka mkoa wa Kivu Kusini, kabla ya Aprili 2024. Katika hatua hii, vituo kadhaa vya jeshi la MONUSCO vitahamishiwa kwa serikali.

Awamu ya pili inahusisha uondokaji wa MONUSCO kutoka Kivu Kaskazini baada ya kujiondoa kutoka Kivu Kusini na mwisho wa tathmini ya awamu ya kwanza ya kuondoka, kama ilivyoombwa na Baraza la Usalama.

Awamu ya tatu itaanza baada ya kukamilika kwa awamu ya 2 na tathmini yake, na itahusisha kujiondoa kikamilifu kutoka jimbo la Ituri.

MONUSCO inasisitiza uamuzi wake wa kutekeleza jukumu lake la kuwalinda raia sanjari na vikosi vya ulinzi na usalama vya Congo.

Mnamo Desemba 19 mwaka 2023, jukumu la MONUSCO liliongezwa upya kwa makubaliano ya mwaka mmoja na Baraza la Usalama na lengo kuu la muda huo ni kuanza kuondoka kwa operesheni hiyo ya MONUSCO.