Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19: Maambukizi yaongezeka kwa asilimia 52 katika mwezi mmoja, yasema WHO

Utoaji wa chanjo aina ya Synovac dhidi ya COVID-19
Unsplash/Mufid Majnun
Utoaji wa chanjo aina ya Synovac dhidi ya COVID-19

COVID-19: Maambukizi yaongezeka kwa asilimia 52 katika mwezi mmoja, yasema WHO

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya, WHO, hii leo limethibisha idadi ya wagonjwa wa COVID-19 duniani kote inaongezeka kwa kasi na kwamba “tutarajie idadi kubwa zaidi ya wagonjwa katika miezi ijayo ya msimu wa baridi kali kwenye maeneo ya kaskazini mwa dunia.”

Takwimu za hivi karibuni kutoka WHO zikijikita katika wiki nne za kuanzia tarehe Novemba hadi Desemba 17 mwaka 2023 zinaonesha ongezeko la asilimia 52 ya idadi ya wagonjwa ikilinganishwa siku 28 zilizotangulia.

Msemaji wa WHO Christian Lindmeier, amewajulisha waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi hii leo kuwa ongezeko hilo ni saw ana wagonjwa wapya 850,000, lakini takwimu kamili zinaweza kuwa za juu.

“Unafahamu kuwa duniani kote na umeshuhudia hata wengi wenu kwenye nchi zetu kwamba utoaji wa taarifa umepungua, vituo vya ufuatiliaji navyo vivyo hivyo, kwingine vimevunjwa kabisa au vimefungwa… kwa hiyo hii bila shaka inatupeleka kwenye kukosa picha halisi na tunatarajia kwa bahati mbaya idadi kubwa zaidi ya wagonjwa kuliko tulivyoripoti,” amesema Bwana Lindmeir.

Maambukizi mengi yamesababishwa aina na mnyumbuliko mpya wa COVIDO uitwao JN.1 ambao kwa sasa unachunguzwa kwa kina na WHO kama mnyumbuliko unaopaswa kufuatiliwa kwa karibu.

Kwa mara ya kwanza aina hiyo  JN.1 ilibainika Marekani kabla ya kusambaa kwenye makumi kadhaa ya nchi.

Inatokana na mnyumbuliko wa COVID uitwao Omicron ambao ulihusishwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya coronavirus">COVID-19 mwaka 2022.