Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 75 ya UDHR: Dumisha uhuru, timiza ahadi ya haki za binadamu

Tamko la kimataifa la haki za binadamu
Credit : Rorie Katz (UNPA stamp designer)
Tamko la kimataifa la haki za binadamu

Miaka 75 ya UDHR: Dumisha uhuru, timiza ahadi ya haki za binadamu

Haki za binadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa viongozi wa dunia kutegemea Tamko la Kimataifa la Haki za Kibinadamu (UDHR) kama mwongozo wa sio tu kutetea haki za binadamu bali pia kuzuia vita, kupambana na chuki, kujenga upya imani na kujenga mustakabali endelevu kwa wote.

 

Katika ujumbe wa video kwa mkutano wa siku mbili unaofanyika huko Geneva, Uswisi leo 11 hadi kesho 12 Desemba, ukiwa ni mkutano wa ngazi ya juu la kuadhimisha miaka 75 ya tamko hilo, Bwana Guterres amekumubushia kwamba hati hiyo muhimu inawasilisha "mwanga wa matumaini" kwa ubinadamu na mwongozo wa uhuru wa kimsingi.

"Tunaposherehekea maadhimisho haya ya 75, natoa wito kwa kila Nchi Mwanachama kutumia fursa hii, na ‘Mkutano wa siku zijazo’ mwaka ujao, kuimarisha kujitolea kwao kwa maadili na kanuni za Azimio la Ulimwengu," amehimiza.

"Hebu tujitahidi kuzingatia na kukuza haki za binadamu, uhuru na usawa - kwa wote. Kwa pamoja, tunaweza kutambua ahadi ya Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu,” ameeleza Guterres. 

‘Ahadi zinazoonekana’

Tukio hilo linajumuisha vikao viwili muhimu vya kuahidi kwa mataifa kutangaza ahadi zinazotekelezeka kuendeleza ulinzi wa haki za binadamu.

Katika mada ‘Sauti katika kutetea haki za binadamu’, washiriki wanatarajiwa kueleza ushuhuda na mitazamo yao kuhusu matokeo ya uwepo wa Tamko la Kiamtaiaf la Haki za Binadamu UDHR. Majadiliano ya jopo pia yatafanyika na wataalam kuchunguza changamoto na kuzingatia kusonga mbele juu ya ulimwengu wote na kutogawanyika kwa haki za binadamu na jinsi ya kuimarisha mfumo wa haki za binadamu.

Kipengele cha viongozi na Wakuu wa Nchi kitafanyika Jumanne, kikifuatiwa na majadiliano kuhusu amani na usalama, teknolojia ya kidijitali, tabianchi na mazingira, na maendeleo na uchumi.

Kushindwa, licha ya maendeleo - Volker Türk

Pia akizungumza kwenye ufunguzi huo, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema kwamba ingawa Tamko la Ulimwengu la Haki za Binadamu limekuwa chanzo cha kuleta mabadiliko ya kijamii duniani kote, miaka 75 iliyopita pia imeshuhudia "kushindwa kwa kiasi kikubwa kutetea haki za binadamu".

“Fikira zangu zinawaendea mamilioni ya watu wanaoteseka katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, hasa Gaza na Israel; nchini Sudani; Ukraine; Myanmar; na maeneo mengine mengi,” amesema Türk.

Bwana Türk ametambua mizizi mbalimbali ya UDHR, ikiwa ni pamoja na majibu ya ulimwengu kwa hofu ya Holocaust, mapinduzi ya Haiti, "maadili makubwa ya Kiafrika ya kutegemeana, ushirikiano na uwajibikaji wa pamoja" na kanuni ya Kiislamu ya zakat, au kuoneana huruma, miongoni mwa wengine.