Korea Kaskazini semeni ukweli na mtende haki kwa watu waliotoweshwa na kutekwa nyara: Türk
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za binadamu Volker Türk hii leo jijini Geneva nchini Uswisi ametoa ripoti ya kina inayoonesha mateso yanayoendelea ya waathirika wa kutoweshwa na kutekwa nyara nchini Korea Kaskazini na kutaka wale wote wanaohusika wachukuliwe hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani ndani ya nchi au mahakama za kimataifa.