Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafa Hanang Tanzania: UN iko bega kwa bega katika usaidizi, asema Milišić

Zlatan_Milišić, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakati wa mahojiano na Stella Vuzo wa UNIC Dar es salaam.
UN Tanzania/Ahimidiwe Olotu
Zlatan_Milišić, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakati wa mahojiano na Stella Vuzo wa UNIC Dar es salaam.

Maafa Hanang Tanzania: UN iko bega kwa bega katika usaidizi, asema Milišić

Tabianchi na mazingira

Wakati mkutano waUmoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 ukiendelea Dubai Falme za Kiarabu, nchini Tanzania mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha yameleta janga la kibinadamu katika wilaya ya Hanang mkoani Manyara Kazkazini mwa nchi hiyo.

Janga hilo limepoteza maisha ya watu, nyumba na miundombinu kuharibiwa, maelfu kutawanywa na kukosa makazi huku watu wengine hawajulikani waliko. Sasa serikali ya nchi hiyo imeomba msaada kwa umoja wa Mataifa ambao umesema uko tayari kusaidia Zlatan Milišić mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo akizungumza na Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam amesema “Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umeshitushwa sana na janga kubwa lililotokea kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo , ambapo hadi sasa imebainika kuwa takriban watu 65 wamepoteza m aisha, zaidi ya 100 wamejeruhiwa na pia cha kusikitisha zaidi ya kaya 1200 sawa na watu wapatao 5000 hadi 6000 wamepoteza nyumba zao.”

Tuko bega kwa bega na serikali ya Tanzania

Kuhusu ombi la serikali ya Tanzania kupata msaada kutoka Umoja wa Mataifa bwana Milišić amesemaUmoja wa Mataifa umekuwa ukifanyakazi na serikali ofisi ya waziri mkuu kuwasaidia na kuimarisha udhibiti wa majanga na hatua za kuyakabili na tunatumai kuna maoni kutokana na juhudi zetu za pamoja katika hatua za haraka na za ufanisi kutoka kwa serikali katika dharura hii. Serikali ilichukua haraka hatua katika siku ya kwanza ya dharura hii, ilisaidia katika operesheni ya kutafita na kuokoa watu , imetoa msaada wa chakula na vifaa vingine kwa watu waliotawanywa.”

Mratibu huyo mkazi ameendelea kusema kwamba “Umoja wa Mataifa umekuwa katika mawasiliano na kuisaidia serikali tangu siku ya kwanza ya kuzuka zahma hii ya dharura, na pia ndani ya UN tumekuwa tukiratibu juhudi kuhusu hatua za kusaidia watu walioathirika na janga hili.”

Tukotayari kusaidia katika tathimini ya janga hili

Kuhusu aina ya msaada ambao wako tayari kuutoa kwa serikali ya Tanzania bwana Zlatan amesemaUmoja wa Mataifa tuko tayari kuisaidia serikali kwa tathimini yoyote ambayo itafanyika na tunaelewa itakuwa hivi karibuni na baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yanajaribu kukusanya rasilimali ili kuwasaidia waathirika kwa misaada. Bila shaka Tanzania inajulikana kwa kutokuwa nchi yenye operesheni za kibinadamu hivyo hatuna rasilimali nyingi kwa haraka , lakini mashirika ya Umoja wa Mataifa yanajaribu kuona nini yanaweza kuchangia na baadhi tayari yameanza kutoka msaada wa chakuna na vitu visivyo chakula. Tunatumai tutaweza kutoa msaada zaidi kadri hali inavyoendelea na kuweza kuisaidia serikali kwa tathimini na matokeo yake.”