Kwa miaka mitatu UNA imepata mafanikio makubwa Tanzania:UNA 

25 Machi 2019

Umoja wa Mataifa umekuwa na mchango mkubwa katika kushirikisha umma wa Tanzania kwenye harakati za uchagizaji na utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs kupitia mbinu mbalimbali ikiwemo mashirika yake na miradi yake. Miongoni mwa mchagizaji mkubwa wa malengo hayo ni UNA.

Jumuiya ya umoja wa Mataifa nchini Tanzania (UNA) imepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa miaka mitatu iliyopita kwa dhamira yakuwa jukwaa la  kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs nchini humo na ushiriki wa vijana.

Akizungumza na Stella Vuzo wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania , UNIC Dar es salaam wakati wa mkutano wa asasi za kiraria jijini Dar es salaam, Renald Maeda Katibu mkuu wa UNA amesema wameweza kutambua umuhimu wa mchango wa vijana, lakini pia kushirikisha Bunge la nchi hiyo

(MAHOJIANO YA STELLA VUZO  NA  RENALD MAEDA)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter