Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaonya, tunapokumbatia teknolojia tuzingatie hatari yake kwa mabadiliko ya tabianchi

Washiriki wa mkutano wa COP28 wakipita katika ukumbi wa Expo City Dubai.
COP28/Walaa Alshaer
Washiriki wa mkutano wa COP28 wakipita katika ukumbi wa Expo City Dubai.

UNESCO yaonya, tunapokumbatia teknolojia tuzingatie hatari yake kwa mabadiliko ya tabianchi

Tabianchi na mazingira

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, leo limetoa ripoti yake ya kwanza kuhusu maadili ya uhandisi wa mabadiliko ya tabianchi likisema kwamba utafiti wa ripoti hiyo unatathmini hatari na fursa za teknolojia mpya za ubadilishanaji na urekebishaji wa masuala ya hali ya hewa na kutoa mapendekezo madhubuti ya utafiti na udhibiti wa tarifa zake.

Shirika hilo limesema sayansi inasaka teknolojia za kuendesha na kurekebisha masuala ya tabianchi, huku shirika hilo likileta mapendekezo ya utafiti na kusimamia uhandisi wake  na kuonya kwamba ukosefu wa maarifa juu ya athari za teknolojia hizi kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi, unaweza kuleta madhara makubwa kwa mfumo ikolojia.

UNESCO imeongwza kwamba mgogoro wa tabianchi unapoendelea na binadamu hushindwa kufikia malengo ya kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa au CO2, uhandisi wa hali ya hewa, unaojulikana pia kama geoengineering, unavutia watu wengi zaidi.

Wanawake nchini Tanzania wakivuna seaweed kama sehemu ya mradi wa kilimo bora cha hali ya hewa.
UN Women/Phil Kabuje
Wanawake nchini Tanzania wakivuna seaweed kama sehemu ya mradi wa kilimo bora cha hali ya hewa.

Mfumo wa ikolojia wa kimataifa

Ripoti hiyo inaakisi juu ya ahadi na hatari kubwa za uingiliaji kati huu mkubwa katika mifumo ya ikolojia ya sayari, iliyotayarishwa na Tume ya Dunia ya UNESCO ya Maadili ya Maarifa ya Sayansi na Teknolojia.

Hati hiyo inajadili teknolojia za uhandisi wa hali ya hewa, zilizogawanywa katika makundi mawili makuu ambayo ni  kuondolewa kwa hewa ukaa, kama vile kufyonza hewa ukaa kutoka kwenye angahewa kupitia miundombinu ya kuivuna au kupnda miti ili kuvyonza hewa ukaa hiyo na kurekebisha mionzi ya jua, kama vile kurudisha mwanga wa jua angani kwa kudachilia chembechembe za erosoli kwenye anga au kupaka rangi nyepesi kwenye nyuzo za maeneo yanayoakisi mwanga.

Ikitathmini hatari hizo, ripoti ya UNESCO inaangazia athari hasi zinazoweza kutokea kwa sera zilizopo za mabadiliko ya tabianchi, kupunguza ufadhili wa kukabiliana na hewa ukaa na vita na udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi. 

Ripoti hiyo pia inaonya kuhusu gharama kubwa na uwezekano wa matumizi ya kijeshi au kijiografia, yanayohitaji utawala bora wa kimataifa.

Athari za ubunifu kwenye hali ya hewa

Zaidi ya hayo, ripoti inaangazia ukosefu wa maarifa kuhusu athari za teknolojia hizi kwa hali ya hewa, ambazo zinaweza kuleta madhara makubwa kwa binadamu, bahari, hali ya joto na viumbe hai.

Matokeo yake, ripoti inapendekeza utafiti mkubwa na kupunguza kutokuwa na uhakika kuhusu vitendo vya mabadiliko ya tabianchi.

Mapendekezo hayo yanajumuisha ulinzi wa lazima wa kisheria wa mataifa, utafiti unaoungwa mkono na viwango vya wazi vya kimaadili na kwa mujibu wa sheria za kimataifa, kuzingatia athari za kuvuka mipaka za maamuzi ya uhandisi wa hali ya hewa, ushirikiano kati ya nchi, na kujumuisha jamii zilizotengwa katika michakato na mengineyo.

UNESCO itawasilisha ripoti hiyo kwa nchi wanachama wake 194 ili kuzingatiwa mjini Dubai wakati wa Mkutano wa Kilele wa mabadiliko ya tabianchi COP28, unaolenga utekelezaji wa kimaadili wa uhandisi wa tabianchi huku kukiwa na uharaka wa kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.