Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mambo 5 unayohitaji kufahamu kuhusu nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani

Wanawake nchini Tanzania wakivuna seaweed kama sehemu ya mradi wa kilimo bora cha hali ya hewa.
UN Women/Phil Kabuje
Wanawake nchini Tanzania wakivuna seaweed kama sehemu ya mradi wa kilimo bora cha hali ya hewa.

Mambo 5 unayohitaji kufahamu kuhusu nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani

Ukuaji wa Kiuchumi

Miaka mitatu baada ya dunia kuwa katika changamoto kubwa ya ugonjwa Covid -19, Umoja wa Mataifa na wadau wengine watakusanyika katika mji mkuu wa Qatar, Doha ili kuja na mkataba mpya wa kihistoria kusaidia nchi ambazo udhaifu wao ndio uliofichuliwa zaidi na janga hili la Covid-19.

Mkutano wa Nchi zenye maendeleo duni au LDCs hufanyika kila baada ya miaka 10 na mkutano wa mwaka huu unaoanza tarehe 5 hadi 9 mwezi huu wa Machi, unaojulikana kama LDC5, utajikita katika kurejesha mahitaji ya nchi 46 katika kilele cha ajenda ya kimataifa na kuwasaidia wakati wanapopambana  kurejea katika mstari wa maendeleo endelwevu. 

Mtoto akiwa ameshikilia sufuria ya nzige katika kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
© UNICEF/Olivia Acland
Mtoto akiwa ameshikilia sufuria ya nzige katika kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

1. Nchi yenye maendeleo duni ni nchi ya namna gani? 

Nchi zenye maendeleo duni (LDCs) ni nchi zilizoorodheshwa na Umoja wa Mataifa ambazo zinaonesha viashiria vya chini kabisa vya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kipato cha mwananchi kwa mwaka katika nchi hizo za LDCs (GNI) ni chini ya dola za kimarekani 1,018; ikilinganishwa na takribani dola  71,000 kwa mwananchi wa Marekani, dola 44,000 nchini Ufaransa, dola 9,900 nchini Uturuki na dola 6,530 nchini Afrika Kusini kwa mujibu watakwimu za Benki ya Dunia. 

Nchi hizi pia zina alama za chini kwenye viashiria vya lishe, afya, uandikishwaji watoto shuleni na kujua kusoma na kuandika na alama za juu za hatari ya kiuchumi na kimazingira, ambayo hupima vipengele kama vile umbali wa watu (kuzifikia huduma), utegemezi wa kilimo na kukabiliwa na majanga ya asili. 

Kwa sasa kuna LDCs 46, nyingi zaidi zikiwa ni nchi za bara la Afrika. Orodha hiyo hupitiwa upya kila baada ya miaka mitatu na Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC. Kati ya mwaka 1994 na 2020 ni nchi sita tu zimemudu kuhitimu (kutoka) katika  orodha ya nchi zenye maendeleo dunia, LDCs. 

Kijiji cha Bikenibeu kusini mwa Tarawa, Kiribati.
© UNICEF/Vlad Sokhin
Kijiji cha Bikenibeu kusini mwa Tarawa, Kiribati.

2. Je, ni changamoto zipi zinazokabili nchi zenye maendeleo duni? 

Hadi kufikia sasa, LDCs 46 ni makazi  ya watu bilioni 1.1, ambayo ni asilimia 14 ya watu wote duniani, na zaidi ya asilimia 75 ya watu hao bado wanaishi katika umaskini. 

Zaidi ya ilivyo kwa nchi nyingine, LDCs ziko katika hatari ya kuzidisha umaskini na kusalia katika hali duni ya maendeleo. Pia wako hatarini kwa majanga ya kiuchumi ya nje, majanga ya asili na yanayosababishwa na wanadamu, magonjwa ya kuambukiza na mabadiliko ya hali ya hewa. 

Hivi sasa, ulimwengu unaelekea kukabiliwa na ongezeko la joto kwa takribani nyuzi joto 2.7 za selsiasi, jambo ambalo linaweza kuzisambaratisha LDCs. Nchi hizi zimechangia kwa uchache zaidi katika utoaji wa hewa ukaa kaboni lakini bado zinakabiliwa na baadhi ya hatari kubwa zaidi kutokana na mabadiliko ya tabianchi. 

Madeni ni tatizo kubwa kwa LDCs zote: 4 zimeainishwa kuwa nchi ambazo ziko katika hatua ya kushindwa kulipa madeni (Msumbiji, Sao Tome and Principe, Somalia na Sudan) na LDCs 16 ziko katika hatari kubwa ya kukumbwa na hali hiyo ya kushindwa kulipa madeni. 

Kwa hivyo, LDCs zinahitaji jicho la karibu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. 

A 5-month-old girl at Paktia Regional Hospital in Gardez, Afghanistan, receives therapeutic milk to treat malnutrition
© UNICEF/Sayed Bidel
A 5-month-old girl at Paktia Regional Hospital in Gardez, Afghanistan, receives therapeutic milk to treat malnutrition

3. Je, Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa zinawezaje kusaidia LDCs?

Juhudi za mfumo wa Umoja wa Mataifa za kurejesha nyuma ongezeko la uwekaji pembeni wa LDCs katika uchumi wa dunia na kuziweka kwenye njia ya ukuaji endelevu na maendeleo zilianzia miaka ya 1960.

Tangu wakati huo, Umoja wa Mataifa umeweka kipaumbele maalum kwa LDCs, kuwatambua kama walio hatarini zaidi katika jumuiya ya kimataifa na kuwapa manufaa fulani ikiwa ni pamoja na:

Ufadhili wa maendeleo: hasa misaada na mikopo kutoka kwa wafadhili na taasisi za fedha.

Multilateral trading system: such as preferential market access and special treatments.

Msaada wa kiufundi: haswa, kuelekea kusaidia biashara.

Mkutano wa kwanza wa LDC ulifanyika Paris, Ufaransa mnamo mwaka 1981 na LDC5, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 50 ulipaswa kufanywa Machi 2022, lakini uliahirishwa hadi mwaka huu 2023 kwa sababu ya coronavirus">COVID-19.

4. Mpango wa Utekelezaji wa Doha ni nini?

Mpango wa Utekelezaji wa Doha (au DPoA, kwa wapenda vifupisho!) ndiyo ramani ya maendeleo ya LDCs iliyokubaliwa Machi 2022.

Inajumuisha maeneo sita muhimu ya kuzingatia:

Kutokomeza umaskini na kujenga uwezo.

Kutumia nguvu za sayansi, teknolojia, na uvumbuzi ili kupambana na udhaifu na kufikia SDGs.

Kusaidia mabadiliko ya kimuundo kama kichocheo cha ustawi.

Kuimarisha biashara ya kimataifa ya LDCs na ushirikiano wa kikanda.

Kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, kupona kutoka kwa janga la COVID-19 na kujenga mnepo dhidi ya majanga yajayo.

Kuhamasisha mshikamano wa kimataifa na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

Utekelezaji kamili wa DPoA utasaidia LDCs kushughulikia janga la COVID-19 na matokeo hasi ya kijamii na kiuchumi na kuziwezesha kurejea kwenye njia ya kufikia SDGs ikiwa ni pamoja na kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa.

Maelezo kamili ya Mpango wa Utendaji wa Doha yanapatikana hapa katika lugha 6 rasmi za Umoja wa Mataifa.