Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takribani watu 2,400 wanazingirwa na maji ya mafuriko yanayoongezeka Jubaland

(Picha ya maktaba) Mji wa Beledweyne umejaa mafuriko baada ya Mto Shabelle kuvunja kingo zake.
© UNICEF
(Picha ya maktaba) Mji wa Beledweyne umejaa mafuriko baada ya Mto Shabelle kuvunja kingo zake.

Takribani watu 2,400 wanazingirwa na maji ya mafuriko yanayoongezeka Jubaland

Msaada wa Kibinadamu

Kwa ombi la Naibu Waziri Mkuu wa Somalia, Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanajitahidi kupata vyombo vya baharini ili kuwawezesha wahudumu kuwahamisha raia katika eneo lililozungukwa na maji huko Jubaland, Ofisi ya moja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu OCHA imethibitisha.  

Stephane Dujarric, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akieleza taarifa hiyo ya OCHA kwa waandishi wa Habari Jumatatu ya leo jijini New York – Marekani, amesema, “sisi, wadau wetu na mamlaka tunahamasisha usaidizi wa haraka ikiwa ni pamoja na chakula, malazi na maji kwa watu walioathiriwa na mafuriko.” 

Mvua za msimu  ambazo zimeanza Oktoba hadi Desemba, sasa zimeongezeka, na mafuriko sasa yanaathiri zaidi ya watu 700,000. 

Zaidi ya watu 110,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kwa muda, huku takriban vifo 25 vimeripotiwa, “hiyo ni kwa mujibu wa wadau wetu wa kibinadamu.” Amesema Dujarric.