Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jimbo la Kusini Magharibi Somalia laaswa kufanya uchaguzi wa amani: UNSOM

Picha za shughuli mbalimbali nchini Somalia.
UN Photo/Ilyas Ahmed)
Picha za shughuli mbalimbali nchini Somalia.

Jimbo la Kusini Magharibi Somalia laaswa kufanya uchaguzi wa amani: UNSOM

Masuala ya UM

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM umetoa wito kwa pande zote husika kenye  uchaguzi ujao wa urais katika Jimbo la  Kusini Magharibi nchini Somalia , kushirikiana  kuhakikisha kuwa mchakato huo unamalizika vizuri na kufuata utaratibu uliowekwa.

Wito huo umetolewa leo mjini Moghadishu  na Mwakilishi Maalum wa Katibu MkuuSomalia na mkuu wa UNSOM, Nicholas Haysom..

Katika taarifa yake mwakilishi huyo amesema, matukio  yaliyaotokea siku chache zilizopita katika eneo hilo yaonyesha kuwepo mgawanyiko kati ya wadau wakuu, kabla ya uchaguzi kufanyika, na kuonya kwamba mgawanyiko huo unaweza kusababisha ghasia na kuongeza kuwa visa vyovyote ambavyo vinakwenda kinyume na sheria zilizowekwa vyaweza  kusababisha vurugu au kutia doa   uaminifu wa mchakato wa uchaguzi.

Bwana Haysom amesema kwa kuwa uchaguzi huu ndio wa kwanza kati ya chaguzi zingine zitakazofanyika  kitaifa mwaka wa 2020, kuna haja ya kuweka mfano bora wa mchakato wa  uchaguzi. Bila shaka washirika wa kimataifa wa Somalia nao walieleza matumaini kama hayo na hofu yao mwezi Novemba mwaka 2016 wakati wa uchaguzi wa wabunge wakati walipowataka wadau wote kushirikiana ili kuwe na matokeo bora.”

Bw. Hayson ana matumaini kuwa viongozi wa Somalia, kama ilivyo kawaida yao, watapata ufumbuzi wa  masuala yahusuyo uchaguzi kupitia mazungumzo.

Bunge la jimbo la Kusini Magharibi litafanya uchaguzi wa rais wa jimbo hilo Novemba 17. Kura kama hizo zitafanyika pia katika majimbo ya Puntland na Jubaland mwaka wa 2019.