Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami yaangazia kupambana na ukosefu wa usawa

Jamii nchini Mauritius wakifanya mazoezi ya kuhama pindi tsunami inatokea.
UNDRR
Jamii nchini Mauritius wakifanya mazoezi ya kuhama pindi tsunami inatokea.

Siku ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami yaangazia kupambana na ukosefu wa usawa

Tabianchi na mazingira

Tarehe 5 Novemba kila mwaka, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami na kaulimbiu ya mwaka huu ni "Kupambana na ukosefu wa usawa kwa mustakabali wenye mnepo".

Katika ujumbe wake kuhusu siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, anakariri kwamba tsunami "ndiyo aina mbaya zaidi ya maafa ya asili".

Athari hata kwa vizazi vijavyo

Kwa mujibu wa Guterres, jambo hili la asili linafichua "kukosekana kwa usawa kwa ukosefu wa usawa uliokita mizizi, na kusababisha madhara makubwa kwa walio hatarini zaidi: watu wenye rasilimali chache, wanaoishi katika jamii zilizotengwa na wale ambao tayari wameathiriwa na machafuko ya tabianchi ambayo hawakusababisha."

Guterres amesisitiza kwamba "athari za tsunami zinaweza kutokea kwa vizazi na vizazi".

Hivi sasa, theluthi moja ya idadi ya watu duniani, hasa katika nchi zilizoendelea kidogo na Nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea, hawajalindwa na mifumo ya tahadhari ya mapema ambayo inaweza kuonya mapema kuhusu tsunami.

Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa ameangazia mpango wa Maonyo ya Mapema kwa Wote, ambao unalenga kulinda idadi ya watu duniani ifikapo mwaka 2027, ukitoa kipaumbele kwa mahitaji ya walio hatarini zaidi.

Maafa ya asili hatari zaidi kuliko yote

Hata hivyo, mpango kazi unahitaji uwekezaji wa dola za Marekani milioni 3.1 katika kipindi cha miaka minne ijayo. Kwa Guterres, hii ni "bei ndogo ya kulinda watu wote dhidi ya hatari zinazoongezeka za tabianchi".

"Kwa kuvunja vikwazo, kukabiliana na ukosefu wa usawa na kukabiliana na janga la tabianchi, tunaweza kujenga ujasiri na kuhakikisha kila mtu ana fursa ya kustawi, hata katika kukabiliana na changamoto kubwa za asili," ameongeza Guterres.

Matukio ya Tsunami ni tishio kubwa kwa kila mtu, lakini ni hatari sana kwa makundi fulani ya watu, kama vile wanawake, watoto, watu wenye ulemavu na wazee.

Lengo kuu la Siku ya Kimataifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami mwaka huu ni kuongeza majadiliano kuhusu kupunguza hatari zinazoletwa na hali hiyo na kuboresha utayari wa jamii.

Ingawa tsunami hazitokei mara kwa mara, zinaweza kuwa na matokeo mabaya. Katika karne iliyopita, kulikuwa na tsunami 58 tu, lakini waathirika walikuwa zaidi ya 260,000.

Kwa wastani, kila janga lilisababisha vifo vya watu 4,600, zaidi ya maafa mengine yoyote ya asili.