Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumfikisha mahakamani mhalifu wa kivita Sheka nchini DR Congo

Kesi ya Ntabo Ntaberi Sheka
MONUSCO
Kesi ya Ntabo Ntaberi Sheka

Kumfikisha mahakamani mhalifu wa kivita Sheka nchini DR Congo

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Kwa saa 96, maagizo yalifuatana. Siku nne baadaye, watu 287 walikufa, wanawake na watoto 387 walibakwa, na vijiji 13 Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, vilivurugwa.

Kesi ya Ntabo Ntaberi Sheka ndiyo kesi ya kitambo na tata zaidi ambayo mahakama katika jimbo la Kivu Kaskazini imewahi kushughulikia, na mwenendo wake na hukumu ya mwisho mwaka 2020 ilitoa mfano mzuri wa jinsi ya kutafsiri mhalifu wa vita mahakamani.

Kabla ya siku ya kimataifa ya Haki ya Jinai ya mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC, ambayo inaadhimisha kupitishwa kwa mkataba wa Roma wa kuanzishwa kwa mahakama hiyo, Habari za Umoja wa Mataifa, UN News imeangalia kwa karibu kesi hiyo inayotoa uchunguzi wa kesi muhimu kwa mataifa yanayotumia haki ya jinai duniani kote.

Pia inaonyesha umuhimu wa msaada unaotolewa na operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa kwa taasisi za haki za kitaifa na usalama.

Uhalifu wa kiwango kisicho na kifani

Muathirika wa ukatili wakingono mjini Goma DRC.
Picha ya UN/Marie Frechon (Maktaba)
Muathirika wa ukatili wakingono mjini Goma DRC.

Tarehe 30 Julai 2010, wafuasi wenye silaha wa wanamgambo wa Nduma Défense du Congo (NDC) walitumwa katika vijiji 13 vya mbali huko Walikale, eneo kubwa zaidi la Kivu Kaskazini, kilomita 150 Magharibi mwa mji mkuu wa mkoa wa Goma.

Likiwa katika msitu mkubwa wa Equatoria, eneo hilo limekumbwa na miongo miwili ya vita, huku makundi mengi yenye silaha yakipigana kudhibiti migodi ya madini yenye faida kubwa, ikiwa ni pamoja na yale madini makuu ya bati yanayochimbwa ya cassiterite.

Bwana Sheka, wakati huo alikuwa na umri wa miaka 34, mchimba madini wa zamani ambaye mwaka mmoja kabla alianzisha kile mwendesha mashtaka mkuu wa kijeshi huko Goma alikiita “kikundi cha wanamgambo wenye kujipanga zaidi" katika eneo hilo, chenye vitengo, vikosi, bataliani na makampuni nay eye ndiye alikuwa akitoa amri ambazo kwa siku nne mchana na usiku, waajiri wake walitekeleza.

"Sheka hakuwa mtu tu," Nadine Sayiba Mpira, mwendesha mashtaka wa umma huko Goma, aliiambia UN News. "Sheka amefanya uhalifu kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana nchini DR Congo".

Tweet URL

Anaeleza jinsi askari wake "walivyokata koo za watu na kuweka vichwa vyao juu ya vigingi na kuandamana katika mitaa ya vijiji wakisema haya ndio vyanakungoja ikiwa hautashutumu kile alichokiita maadui".

Tarehe 2 Agosti 2010, wanamgambo wenye silaha walianza kumiliki kikamilifu vijiji.

Hati ya kusakwa kwa uhalifu wa kivita

Wale ambao waliweza walikimbilia mahala pa usalama. Baadhi walitafuta msaada wa kimatibabu kutoka kwa shirika la jirani lisilo la kiserikali (NGO).

Ndani ya wiki mbili, maelezo ya manusura yalifika kwa mamlaka. Vyombo vya habari viliyaita mashambulizi hayo "ubakaji wa halaiki". 

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, uliunga mkono kutumwa kwa kikosi cha polisi.

Mwezi Novemba 2010, malalamiko yaliwasilishwa dhidi ya kiongozi huyo wa vita. 

Kisha mamlaka ya Congo ilitoa hati ya kukamatwa kwa Bwana Sheka kitaifa, na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilimuongeza kwenye orodha yake ya vikwazo.

Ikiwa na jukumu la kulinda raia na kuunga mkono mamlaka za kitaifa, MONUSCO ilizindua “Operesheni Silent Valley” mapema Agosti 2011, ili kusaidia wakazi kurejea salama katika vijiji vyao.

Hakuna chaguo jingine ila kujisalimisha

Bwana Sheka sasa alikuwa mtoro. "Akiwa amezungukwa kutoka pande zote, sasa alikuwa amedhoofika na hakuwa na la kufanya ila kujisalimisha," amesema Kanali Ndaka Mbwedi Hyppolite, mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya kijeshi ya Kivu Kaskazini, iliyosikiliza kesi hiyo. 

Mheshimiwa Sheka lijisalimisha Julai 26 mwaka 2017 kwa MONUSCO, ambayo ilimkabidhi kwa mamlaka ya Congo, ambayo nayo ilimfungulia mashtaka ya uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na mauaji, utumwa wa ngono, kuajiri watoto vitani, uporaji na ubakaji.

"Sasa ulikuwa wakati wa kusema ukweli na kukabiliana na matokeo ya ukweli," Bi Sayiba alisema.

Mhalifu wa kivita na wa dhidi ya ubinadamu Ntabo Ntaberi Sheka muasisi na kiongozi wa  Nduma Défense of Congo (NDC) Kivu Kaskazini nchini DRC
MONUSCO
Mhalifu wa kivita na wa dhidi ya ubinadamu Ntabo Ntaberi Sheka muasisi na kiongozi wa Nduma Défense of Congo (NDC) Kivu Kaskazini nchini DRC

Kesi: nakala 3,000 za ushahidi

Kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, walinda amani wa Umoja wa Mataifa walisaidia kujenga mahabusu aliyokuwa akiishi Bwana Sheka na chumba chenyewe cha mahakama, ambapo kesi za mahakama ya kijeshi zilifanyika kwa muda wa miaka miwili, zilisitishwa kuanzia Machi hadi Juni 2020 kutokana na kuanza kwa janga la coronavirus">COVID-19.

Kufikia Novemba 2018, mahakama ilipitia ushahidi 3,000 na kusikiliza mashahidi 178 katika kesi 108.

Ushahidi wao ulikuwa na jukumu muhimu, ukiwakilisha hatua ya mwisho ya mwendesha mashtaka kuthibitisha kwamba uhalifu umetendwa, alielezea Patient Iraguha, mshauri mkuu wa kisheria wa TRIAL International nchini DRC, ambaye alisaidia mamlaka katika kesi hiyo .

Lakini kupata waathirika kutoa ushahidi ilikuwa kibarua kigumu waendesha mashtaka wa Congo walisema.

Wakati wa kesi hiyo, Bwana Sheka aliwasiliana na baadhi ya waathiriwa ili kuwatisha na hivyo kuhatarisha utashi wao wa kufika mahakamani. Hata hivyo, juhudi za pamoja zilizohusisha Umoja wa Mataifa na washirika kama TRIAL International zilibadilisha hilo, alisema Bi Sayiba.

Kesi ya Ntabo Ntaberi Sheka.
MONUSCO
Kesi ya Ntabo Ntaberi Sheka.

Kanali Ndaka aliafiki na kuongeza kuwa baadhi ya waathiriwa wa ubakaji pia wanahofia kunyanyapaliwa na jamii.

Hatua za ulinzi ziliwekwa na mamlaka za mahakama ziliweza kukusanya ushahidi kwa kushirikiana na MONUSCO, ambayo pia ilitoa mafunzo kwa mahakama kuhusu taratibu za sheria za kimataifa za makosa ya jinai, hivyo kuipa mahakama ujuzi wa kutosha kuchunguza kesi hiyo ipasavyo, alisema.

Ameongeza kuwa "Wakati mamlaka ya Congo ilibidi kwenda shambani kuchunguza au kusikiliza waathirika, walizingirwa na kikosi cha MONUSCO. Waathirika waliojitokeza walifanya hivyo kutokana na msaada uliotolewa na washirika wetu."

Kesi ya Ntabo Ntaberi Sheka
MONUSCO
Kesi ya Ntabo Ntaberi Sheka

Tonderai Chikuhwa, mkuu wa wafanyikazi katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo anakumbuka kusikia bayana juu ya uhalifu huo.

"Shuhuda za kuhuzunisha nilizosikia kutoka kwa walionusurika katika vijiji 7 kuanzia Kibua hadi Mpofu hadi Walikale mwaka 2010 hazifutiki akilini mwangu," aliandika kwenye mtandao wa kijamii wakati huo.

Mashahidi wa kwanza kufika mahakamani walikuwa watoto sita, huku waathirika hao wakitoa ushahidi wao hadi Julai 2020.

"Baada ya kutoa ushuhuda wake kwa mahakama, Sheka alianza kulia," anakumbuka Bi Sayiba.

Alisema "Machozi ya mshtakiwa ni jawabu. Nafikiri Sheka aligundua kuwa sasa yuko peke yake na ilibidi awajibike kwa matendo yake.”

Uamuzi: Congo ilitekeleza haki

Mnamo 23 Novemba 2020, mahakama ya uendeshaji ya kijeshi ilimhukumu Bwana Sheka kifungo cha maisha jela.

"Hii inaashiria hatua muhimu kuelekea mbele katika vita dhidi ya ukwepaji wa sheria kwa wahalifu wa kuajiri watoto jeshini na ukiukaji mwingine mkubwa wa haki," aliandika Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kesi hiyo katika ripoti yake inayohusu watoto na migogoro ya silaha nchini DRC.

Bi Sayiba amesema hukumu hiyo ilituma "ujumbe mkubwa na hakikisho kwa waathirika ambao sasa wanaweza kuona kwamba ushahidi wao haukuwa bure".

Kwa kanali Ndaka, anasema hukumu hiyo ilikuwa "chanzo cha fahari kwangu, kwa nchi yangu, kwa haki ya Congo".

Leo hii, Umoja wa Mataifa unaendelea kuunga mkono juhudi za kukomesha hali ya ukwepaji sheria nchini DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Mali, Sudan Kusini na katika nchi nyingine. 

Kesi ya Ntabo Ntaberi Sheka.
MONUSCO

Huko Kivu Kaskazini, ofisi ya mwendesha mashtaka iliongezwa wigo mwezi Juni, kwa msaada wa Umoja wa Mataifa, hadi kwenye mahakama ya amani ya Goma.

Bwana Sheka, ambaye sasa ana umri wa miaka 47, anatumikia kifungo chake cha maisha katika gereza moja kwenye mji mkuu, Kinshasa.

Kanali Ndaka amesema "Ukweli kwamba Sheka amehukumiwa na kuhukumiwa ni dhibitisho kwamba utawala wa sheria upo na kwamba huwezi kukwepa sheria wakati umefanya uhalifu mkubwa na wa kutisha. Haki ya Congo iliweza kufanya hivyo, kwa nia, dhamira na njia. Ilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo na ilifanya.”