Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN imelaani vikali shambulio lililoua na kujeruhi wafanyakazi wa ukoaji Kherson Ukraine

Mwanamke akitolewa katika kitongoji cha Kherson kilichofurika baada ya kuharibiwa kwa bwawa la Kakhovka kusini mwa Ukrainia.
© UNICEF/Alexsey Filippov
Mwanamke akitolewa katika kitongoji cha Kherson kilichofurika baada ya kuharibiwa kwa bwawa la Kakhovka kusini mwa Ukrainia.

UN imelaani vikali shambulio lililoua na kujeruhi wafanyakazi wa ukoaji Kherson Ukraine

Amani na Usalama

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine Matthew Hollingworth amelaani vikali shambulio lililofanywa na Urusi kwenye eneo la Kherson lililoathirika vibaya na mafuriko ya bwawa la Kakhovka, na kukatili maisha ya mfanyakazi wa ukoaji na kujeruhi wengine. 

Katika tarifa yake iliyotolewa leo mjini Kyiv  Ukraine mratibu huyo Hollingworth amesema “Inasikitisha sana kwamba waokoaji wameuawa na kujeruhiwa jana huko Kherson walipokuwa wakisaidia jamii zilizoathiriwa na uharibifu mkubwa wa bwawa la Kakhovka.”

Kwa mujibu wa duru za habari mfanyakzi mmoja wa uokoaji wa ofisi ya huduma za dharura za Ukraine ameuawa katika shambulio hilo wakati waokoaji wengine wanane wamejeruhiwa huku sita wakielezwa kuwa katika hali mbayá.

Imeleezwa kuwa shambulio hilo lililtokea wakati vikosi vya jeshi la Urusi vilipowafyatulia risasi wafanyakazi hao wa uokoaji wakiwa wakiwa katika operesheni za kusafisha matope yaliyotokana na uharibifu katika bwawa la Kakhovka.

Kwa niaba ya jumuiya ya masuala ya kibinadamu bwana Hollingworth ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na kuwatakia majeruhi wote ahuweni ya haraka akiongeza kuwa “Fikra zetu pia ziko na ofisi ya huduma za dharura za Ukraine, inayofanya kazi katika mazingira magumu sana kusaidia watu wake.”

Mratibu huyo wa masuala ya kibinadamu amekumbusha kuwa “Tukio hili ni mfano mwingine wa athari mbayá za kibinadamu za uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.” 

Na amesisitiza kwamba raia wote wakiwemo wafanyakazi wa ukoaji wanalindwa chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu na kuwashambulia na kuwaua ni jambo lisilokubalika.