Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kati ya watoto 10 wanaozaliwa, 1 ni njiti na kila sekunde 40, mtoto 1 kati ya hao hufariki dunia

Mhudumu wa afya akimuweka mtoto mchanga ndani ya eneo maalumu lenye joto lililopimwa (incubator) ili kuboresha uwezekano wa kuishi. Picha: IRIN/Sean Kimmons
Photo: IRIN/Sean Kimmons
Mhudumu wa afya akimuweka mtoto mchanga ndani ya eneo maalumu lenye joto lililopimwa (incubator) ili kuboresha uwezekano wa kuishi. Picha: IRIN/Sean Kimmons

Kati ya watoto 10 wanaozaliwa, 1 ni njiti na kila sekunde 40, mtoto 1 kati ya hao hufariki dunia

Afya

Makadirio yanaonesha kwamba mwaka 2020 takriban watoto milioni 13.4 walizaliwa kabla ya muda yaani njiti, huku karibu milioni 1 kati yao wakifariki kutokana na matatizo yanayotokana na hali hiyo ya kuzaliwa kabla ya wakati. 

Ripoti hiyo iliyopewa usiku wa kuamkia leo Mei 10 ikiwa na jina Kuzaliwa njiti: muongo wa hatua dhidi ya kuzaliwa kabla ya wakati, iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) pamoja na PMNCH ambao ni Ushirikiano wa mkubwa zaidi unaoangazia afya ya Mama, watoto na vijana inafafanua kuwa .  

Ripoti hiyo inajumuisha makadirio yaliyoboreshwa kutoka WHO na UNICEF, yaliyotayarishwa na London School of Hygiene and Tropical Medicine, kuhusu uwepo wa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati. Kwa ujumla, inagundua kuwa viwango vya kuzaliwa kabla ya wakati havijabadilika katika eneo lolote duniani katika muongo mmoja uliopita, na watoto milioni 152 walio katika mazingira hatarishi walizaliwa hivi karibuni kutoka mwaka 2010 hadi mwaka 2020. 

Kuzaliwa kabla ya wakati sasa ndio sababu kuu ya vifo vya watoto, ikichukua zaidi ya kifo 1 kati ya vifo 5 vya watoto vinavyotokea kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano baada ya kuzaliwa. Watoto njiti wanaonusurika wanaweza kukabiliwa na changamoto ya afya ya maisha yote, pamoja na kuongezeka kwa uwezekano wa ulemavu na ucheleweshaji wa maendeleo. 

Pengo la usawa 

Kutokana na ripoti yamwaka 2012 kuhusu suala hili, ripoti hii mpya inatoa  muhtasari wa kina wa kuenea kwa kuzaliwa kabla ya wakati na athari zake kwa wanawake, familia, jamii na uchumi. 

Mara nyingi, eneo ambako watoto huzaliwa huamua ikiwa wataishi au la. Ripoti hiyo inabainisha kuwa katika nchi zenye kipato cha chini ni mtoto 1 tu kati ya 10 wanaozaliwa njiti (chini ya wiki 28) wanaofanikiwa kuishi ikilinganishwa na zaidi ya 9 kati ya 10 katika nchi zenye kipato cha juu. Ukosefu wa usawa wa pengo unaohusiana na rangi, kabila, mapato na ufikiaji wa huduma bora huamua uwezekano wa kuzaliwa kabla ya wakati, kifo na ulemavu, hata katika nchi zenye kipato ya juu. 

Kusini mwa Asia na Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara ndizo zina viwango vya juu zaidi vya kuzaliwa kabla ya wakati, na watoto wachanga katika maeneo haya wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya vifo. Kwa pamoja, maeneo haya mawili yanachangia zaidi ya asilimia 65 ya watoto wanaozaliwa njiti. Ripoti hiyo pia inaangazia kwamba athari za migogoro, mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira, COVID-19, na kupanda kwa gharama za maisha kunaongeza hatari kwa wanawake na watoto kila mahali. Kwa mfano, uchafuzi wa hewa unakadiriwa kuchangia watoto milioni 6 kuzaliwa njiti kila mwaka. Takriban mtoto 1 kati ya 10 anayezaliwa kabla ya wakati anazaliwa katika nchi 10 zilizo dhaifu zaidi zilizoathiriwa na majanga ya kibinadamu, kulingana na uchambuzi mpya katika ripoti hiyo. 

Hatari za afya ya uzazi, kama vile mimba za utotoni na shinikizo kubwa la damu wakati wa ujauzito (pre-eclampsia), zinahusishwa kwa karibu na kuzaliwa njiti. Hii inasisitiza haja ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya ya ya kujamiina nay a uzazi, ikiwa ni pamoja na upangaji uzazi bora, na uangalizi wa hali ya juu wakati wa ujauzito na wakati wa kuzaliwa. 

Ajenda ya utekelezaji: uwekezaji zaidi na harakati za kijamii 

Muongo uliopita pia umeshuhudia ukuaji wa uharakati wa jamii kuhusu uzazi wa kujifungua kabla ya wakati na uzuiaji wa mtoto kufia tumboni, ikiendeshwa na mitandao ya wazazi, wataalamu wa afya,  

Ulimwenguni kote, vikundi vya familia zilizoathiriwa za kuzaliwa kabla ya wakati vimekuwa mstari wa mbele kutetea upatikanaji wa utunzaji bora na mabadiliko ya sera na kusaidia familia zingine. 

WHO, UNICEF, UNFPA na PMNCH wanatoa wito wa kuchukua hatua zifuatazo ili kuboresha huduma kwa wanawake na watoto wachanga na kupunguza hatari za kuzaliwa kabla ya wakati au njiti: 

Ongezeko la uwekezaji: Kuhamasisha rasilimali za kimataifa na za ndani ili kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga, kuhakikisha uangalizi wa hali ya juu unatolewa wakati na pale unapohitajika. 

Utekelezaji ulioharakishwa: Kufikia malengo ya nchi kwa ajili ya maendeleo kupitia utekelezaji wa sera zilizowekwa za kitaifa za uangalizi wa uzazi na watoto wachanga. 

Ushirikiano katika sekta zote: Kukuza elimu kupitia mzunguko wa maisha; kusaidia uwekezaji nadhifu wa kiuchumi, kwa ufadhili wa pamoja katika sekta zote; kuimarisha majibu ya kukabiliana na hali ya hewa katika kipindi chote cha maisha; na kuendeleza uratibu na uthabiti wa mifumo ya dharura. 

Ubunifu unaoendeshwa ndani ya nchi: Kuwekeza katika uvumbuzi na utafiti unaoongozwa ndani ya nchi ili kusaidia uboreshaji wa ubora wa utunzaji na usawa katika ufikiaji.