Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za ukame Pembe ya Afrika, WHO na wadau waingilia kati kupambana na utapiamlo mkali

Ukame Pembe ya Afrika umesababisha utapiamlo kwa watoto Karamoja nchini Uganda
Picha: WHO Video screenshot
Ukame Pembe ya Afrika umesababisha utapiamlo kwa watoto Karamoja nchini Uganda

Athari za ukame Pembe ya Afrika, WHO na wadau waingilia kati kupambana na utapiamlo mkali

Tabianchi na mazingira

Karomoja, moja ya mikoa nchini Uganda, kaskazini mashariki mwa nchi, Uganda inakopakana na Sudan na Kenya kama ilivyo kwa maeneo mengine katika ukanda huo wa Pembe ya Afrika, nako kumeathiriwa na ukame mkali na hivyo kuyumbisha upatikanaji wa chakula.

Hapa panaonekana vijumba vidogo vidogo vya msonge vilivyojengwa kwa matofali ya udongo, vimeezekwa kwa nyasi na kushikizwa kwa miti pembezoni.

Kama ilivyo kwa msichana yeyote mdogo wa umri wa miaka 7, Magdalena Akwii anapenda kucheza. Lakini miezi sita iliyopita wapendwa wake walikuwa na hofu kuhusu maisha yake.

“Niliona namna msichana alikuwa hayuko sawa.Anaanza kueleza Asio Sarah Maria, mama mdogo wa Akwii. Anaendelea kueleza kuwa mwili wa Magdalena ulikuwa umekonda, una vipele na kwa hiyo wakampeleka Magdalena kwenye kituo cha afya ambako walimpima uzito na pia wakampima mzingo wa mkono katikati ya bega na kiwiko.

Magdalena aligundulika kuwa na utapiamlo mkali na hivyo akapewa aina fulani ya vyakula tiba ambavyo vinakuwa tayari kuliwa wakati wowote na ambavyo vinasaidia kuongeza uzito haraka kwa watoto wenye utapiamlo mkali.

“Hivi sasa wauguzi wana furaha.” Anaendelea kueleza mama mdogo wa Magdalena akieleza kuwa sababu ya wauguzi kuwa na furaha ni kwamba mara ya mwisho Magdalena Akwii alipopimwa mzigo wa mkono, kipimo kilionesha rangi nyekundu lakini sasa hali ni nzuri, kipimo kinaonesha rangi ya kijani.

Ukame Pembe ya Afrika umesababisha utapiamlo kwa watoto Karamoja nchini Uganda
Picha: WHO Video screenshot
Ukame Pembe ya Afrika umesababisha utapiamlo kwa watoto Karamoja nchini Uganda

WHO inasema katika eneo la pembe ya Afrika, watoto 92,000 kama Magdalena Akwii katika eneo la Karamoja, wanahitaji huduma ya kuokoa maisha yao lakini kukosekana kwa mafunzo na vifaa vinavyohitajika kufanyia vipimo na kutibu utapiamlo mkali kulikuwa kunawakatisha tamaa wahudumu wa afya hadi pale WHO na wadau wake walipoingilia kati.

Otita Joseph ni Mwenyekiti wa eneo la Lupa anathibitisha hilo akisema,

“Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni limefanya mengi hapa. Kwa sababu wanatoa usaidizi kuanzia wilayani hadi kwenye kata.”

Na sasa, Akwii Magdalena ambaye tumemwangazia tangu mwanzo, sasa akiwa tayari ana afya nzuri anaweza kucheza kama watoto wengine.